Home Uncategorized KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA

KANTE NA JORGINHO WAPO KWENYE MPANGO WA KUUZWA


FRANK Lampard, Kocha Mkuu wa Chelsea inaelezwa kuwa yupo kwenye mpango wa kumuuza N’Golo Kante na Jorginho.

Inaelezwa kuwa mpango wa Chelsea ni kupata saini ya Hakim Ziyech wa Ajax na Timo Werner anayekipiga RB Leipzig hivyo wanataka mkwanja wa kuwalipa wachezaji hao.

Licha ya kueleza kuwa kuwauza wachezaji wote wawili kwa wakati mmoja ambao ni viungo ni hatari kwa Chelsea bado mabosi hao wanaamini haitakuwa tatizo kwao mahitaji yao makubwa ni kupata mkwanja.

Jorginho anaweza kuibukia ndani ya Juventus huku Kante akitajwa kuweza kuibukia ndani ya Klabu ya PSG.

SOMA NA HII  SIMBA WAPIGA MATIZI YA MWISHO LEO, VITA YAO KESHO INA VIGINGI VIKALI MBELE YA MBEYA CITY

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here