Home Habari za michezo WASAUZI WAJITOSA KWA FEI TOTO…SIMBA NA AZAM WAKICHUNGULIA ISHU YAKE NA YANGA...

WASAUZI WAJITOSA KWA FEI TOTO…SIMBA NA AZAM WAKICHUNGULIA ISHU YAKE NA YANGA ILIVYO…

Tetesi za Usajili Yanga

Wakati kamati ya hadhi za wachezaji ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) likisisitiza kuwa Feisal Salum “Feitoto” ni mali ya Yanga SC, klabu ya soka inayoshiriki ligi kuu nchini Afrika Kusini (PSL) Sekhukhune United imeanza mazungumzo na wawakilishi wa kiungo huyo wa timu ya taifa ya Tanzania.

Inasemekana mazungumzo kati ya klabu hiyo pamoja na wawakilishi wa Feisal Salum yameanza na klabu hiyo inamhitaji kiungo huyo ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha timu hiyo.

Sekhukhune United waliomaliza wakiwa nafasi ya saba(7) kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Afrika Kusini wanatumia uwanja wa Peter Mokaba Stadium uliopo kwenye jiji la Polokwane.

Hawa wameanza maboresho ya kikosi chao kuelekea msimu ujao na tayari wameanza mazungumzo na wawakilishi wa Feisal Salum “Feitoto”.

Hata hivyo taarifa za awali zinasema kuwa klabu za Simba na Azam pia zinammendea kiungo huyo ambaye amekuwa hana wakati mzuri na klabu yake kwa msimu huu.

Tetesi za usajili bongo zinadai kuwa toka mwanzoni mwa sakata lake na Yanga kuanza katikati ya msimu huu, klabu hizo zilijiweka katika nafasi ya kumpata mchezaji huyo kwa namna yoyote ile.

SOMA NA HII  ULE MSELELEKO WA DStv SAFARI HII UNAENDA NA WATOTO AISEE....MTONYO NI ULE ULE NA CHANELI NI ILE ILE...