Home Habari za michezo KIUNGO MNIGERIA AJIPELEKA ‘KIAINA’ YANGA SC….AFUNGUKA KUSHINDWANA NA SIMBA ….

KIUNGO MNIGERIA AJIPELEKA ‘KIAINA’ YANGA SC….AFUNGUKA KUSHINDWANA NA SIMBA ….

Habari za Simba SC na Yanga SC

KIUNGO wa Rivers United ya Nigeria, Morice Chukwu amekiri kwamba kuna uwezekano mkubwa mwezi Julai mwaka huu akawa kwenye uzi wa njano au mwekundu ndani ya ardhi ya Tanzania.

Staa huyo ambaye anacheza kama kiungo mshambuliaji na mkabaji, amefichua mazungumzo yake na Kocha wa Simba,Robert Robertinho na jinsi Nasreeden Nabi wa Yanga SC alivyomuita chemba baada ya mechi ya juzi Jumapili usiku.

Mchezaji huyo anasema awali baada ya mechi yao na Yanga nchini Nigeria alizungumza na Robertinho na baadhi ya watu waliosema wao ni Simba SC, lakini hawakufikia muafaka, baada ya mechi ya Dar es Salaam Nabi nae akamuambia nia yake ya kutaka kumsajili Jangwani.

Morice ambaye alianza kuitumikia Rivers United mwaka 2021, alisema; “Nilizungumza na Kocha wa Simba kwanza kuhusiana na kujiunga na timu hiyo msimu ujao, lakini hata Yanga baada ya mechi yetu Kocha wao alinifuata tukazungumza, kwa jinsi ninavyoona nitakuja Dar es Salaam Julai.”

“Ninaweza kusaini Simba SC au Yanga SC, mpaka baadhi ya mashabiki wananiambia lazima uje, mimi sina tatizo, kuna uwezekano mkubwa nikasaini moja kati ya hizi timu mbili kwavile nimezungumza na makocha wao mambo mengi,”alisema Morice.

Simba SC na Yanga SC zimeanza kufanya usajili wa kimyakimya kujipanga kwaajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa. Watani hao wa jadi tayari wana uhakika wa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao kupitia ofa ya Caf ambayo imeipa Tanzania nafasi nne za uwakilishi.

SOMA NA HII  WAKATI WAARABU WAKITAJWA KUMTAKA MAYELE....BOSI YANGA AONYESHA JEURI YA PESA...