Home Yanga SC REKODI YA SIMON MSUVA BADO INAISHI YANGA

REKODI YA SIMON MSUVA BADO INAISHI YANGA


REKODI ya nyota wa zamani wa Yanga mzawa kuwa namba moja kwa utupiaji katika msimu wa 2016/17 imekuwa ngumu kuvunjwa mpaka sasa kwa kuwa wazawa wengi wamekuwa wakikwama kuwa namba moja kwenye utupiaji.

Ilikuwa ni msimu wa 2016/17 nyota huyo alitupia kibindoni jumla ya mabao 14 na alisepa na kiatu cha ufungaji bora. Wakati huo Msuva  ambaye ni mzawa alifunga mabao hayo sawa na nyota ambaye yupo Ruvu Shooting, Abrahaman Mussa ambaye naye alifunga mabao hayo.

Kwa sasa Msuva hayupo ndani ya ardhi ya Bongo yupo zake anakipiga ndani ya Wydad Athletic Club huku Abrahaman akiendelea kusalia ndani ya Ruvu.

Msimu wa 2017/18 mtupiaji namba moja alikuwa ni Obrey Chirwa raia wa Zimbabwe ambaye alitupia jumla ya mabao 12. Chirwa msimu wa 2020/21 alikuwa ndani ya Azam FC ambapo alitupia mabao matano.

Kwa sasa Chirwa ni mchezaji huru baada ya dili lake kumeguka ndani ya Azam FC ambao wametangaza rasmi kuachana naye hivyo hatakuwa katika kikosi hicho msimu wa 2021/22.

2018/19 alikuwa ni Heritier Makambo, raia wa Congo mzee wa kuwajaza ambaye alitupia jumla ya mabao 17. Alisepa na kuibukia Klabu ya Horoya ya Guinea ila kwa sasa amerejea tena msimu wa 2021/22 anatarajiwa kuendelea kasi yake ndani ya Yanga. 

2019/20 mfungaji bora alikuwa ni David Molinga ambaye alitupia jumla ya mabao 11 mkataba wake ulipomeguka alisepa ndani ya Yanga yeye ni raia wa Congo.

Kwa msimu wa 2020/21 mfungaji namba moja ni Yacouba Songne raia wa Burkina Faso ambaye alitupia jumla ya mabao nane na alikuwa na pasi nne za mabao.


SOMA NA HII  DILI LA MAHOP LAINGIA MDUDU, HUKU CAF IKITOA SIKU TATU TU KWA YANGA, ISHU IKO HIVI