Home Habari za michezo DILI LA MAHOP LAINGIA MDUDU, HUKU CAF IKITOA SIKU TATU TU KWA...

DILI LA MAHOP LAINGIA MDUDU, HUKU CAF IKITOA SIKU TATU TU KWA YANGA, ISHU IKO HIVI

Habari za Yanga

dili la mshambuliaji Mcameroon, Emmanuel Mahop limeingia mdudu na limebakiza sekunde chache kabisa kuishia njiani. Amewagawa mabosi wa Yanga ambapo wengi wameingiwa mashaka haswa wakiangalia video zake na kufikiria mitetemo ya Fiston Mayele.

Hata matakwa yake makubwa ni vitu ambavyo vimewafanya wamuone wa kawaida sana lakini wana mtihani wa kumaliza utata huo ndani ya siku tatu tu. Caf wamebakiza siku tatu kufunga usajili wao, wakichelewa hapo watalazimika kutumia wachezaji waliopo sasa pale mbele.

Yanga imekaa mezani na Mahop ambaye ni mfungaji bora wa Cameroon, lakini wameshindwa kukubaliana mambo mawili kwanza wakiweka wasiwasi juu ya ubora wake hasa kuchukua nafasi ya Fiston Mayele ambaye wakati wowote kuanzia wiki ijayo atatimka nchini kuelekea Pyramid ya Misri.

Endapo Yanga itashindwa kupata mwafaka wa mshambuliaji huyo watalazimika kuingia kwenye mechi za awali na washambuliaji walionao sasa Kennedy Musonda, Crispin Ngushi na Clement Mzize.

Yanga ikikosa kusajili mshambuliaji sasa italazimika kusubiri hadi kujua hatma yao ya kuingia hatua ya makundi na ndio wataweza kuingiza jina lingine jambo ambalo litakuwa hatari sana kwao.

Mabosi wa Yanga wanaona kuna namna wanatakiwa kujiridhisha zaidi juu ya ubora wa Mahop licha ya takwimu zake za msimu uliopita kuwa bora akifunga mabao 15 katika mechi 20 na kuonyesha kuwashawishi.

“Tunataka kujiridhisha zaidi juu ya hilo kwa hiyo tumeona tujipe nafasi, unajua presha kubwa iliyopo hapa tunatafuta mtu anayekuja kuchukua nafasi ya Fiston Mayele ambaye wote tunajua juu ya ubora wake,” alisema bosi huyo wa juu na kukiri kwamba uwezekano wa kuachana na dili hilo ni mkubwa.

Ukiacha suala la ubora, hatua ya mshambuliaji huyo kuwagomea mara mbili mezani mabosi wa Yanga kushusha fedha anazotaka za usajili akitaka fedha nyingi pia limetajwa kuwashtua vigogo hao na kuamua kufikiri tofauti.

Taarifa mpya ya ndani zaidi ni vigogo hao wamerudi sokoni upya wakiangalia kama kuna mtu wa maana wanaweza kumsaka kuja kuingia katika kikosi chao huku wengine wakishauri mchakato huo usiharakishwe ili kukwepa kupata mshambuliaji asiyekuwa na ubora lakini hakuna namna.

SOMA NA HII  WAKATI WENZAKE WAKIKAA SAWA ...PHIRI AZIDI KUSOTA SIMBA...MBRAZILI AMTUPA NNJE...

1 COMMENT

  1. Hakika naipenda YANGA star ila mbn sas tuko vizuri san sis atuongop vitisho vyovyote t tumetimia kwa kila kitu sisi ndio wana wa jangwan YANGA AFRECK😍😍😍😍😍