KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Saido Ntibazonkiza amesema kipaombele chake cha kwanza kupata matokeo na kuvuna pointi tatu baada ya hapo atafikiria suala la kuwania tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2022/23.
Simba juzi iliibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye dimba la Azam Complex, katika mchezo Saido Ntibazonkiza amefunga mabao tano kati ya sita na kiungo huyo.
Ntibazonkiza ameingia katika vita na Mayele katika kuwania kiatu dhahabu amefikisha maboa 14 ya ligi mpaka sasa akizidiwa moja na kinara wa mabao Fiston Mayele akiwa na mabao 16 huku mchezo mmoja ukiwa umebakia.
Simba ikiwa katika kampeni kubwa ya nyota huyo kumalizia vizuri katika mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union kwa Ntibazonkiza kushinda bao zaidi ya moja ili kufanikiwa malengo yao ya kuwaa ufungaji bora kwa msimu huu wa 2022/23.
Ntibazonkiza alisema lengo la kwanza ni kusaidia timu na kuhusu kiatu cha dhahabu kitafuata baada, jambo la umuhimu ni kusaidia timu kupata ushindi na kucheza vizuri ikitokea amefanikiwa kupata kiatu cha dhahabu itakuwa jambo jema na la furaha.
“Namshukuru Mwenyez Mungu tumefanikiwa kupata ushindi mnono , kwangu Simba ndio kitu cha kwanz kuhusu kuibuk mfungaji bora itakuwa ziada ingawa nitafurahi ikitokea..
Natambua uwezo wa Mayele ni mchezaji mzuri lakini kwa sasa naangalia timu yangu kuona tunamaliza ligi kwa heshima,” alisema Ntibazonkiza.
Kiungo huyo amekuwa mchezaji wa kwanz kufunga mabao matano kwenye mchezo mmoja katika historia ya Ligi ya Tanzania huku ameweka rekodi nyingine ya kufunga hat trick 2 katika msimu mmoja.
Naye Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alisema wanatafuta tuzo ya mchezaji mmoja mmoja na msimu huu wanahitaji kiatu cha ufungaji bora baada ya msimu ujao kukosa.
Alisema msimu ujao kiatu kilienda kwa George Mpole, sasa wanahitaji kwenda Simba kupitia mchezaji wao Ntibazonkiza hilo litadhihirisha kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Coastal Union.
“Suala la mchezaji bora halina ubishi Ntibazonkiza anachukuwa kwa sababu ya takwimu , kuhusu ufungaji bora hii ni kampeni na jambo la kitaifa nyota huyo kuwatwaa kiatu hicho,” alisema Ahmed.
Leo Simba watakuwa kwenye dimba la Uhuru kuikaribisha Coastal Union katika mechi ya kufunga pazia la ligi kuu ya NBC msimu wa 2022/23.
Katika mchezo huo unatazamiwa kuwa wa ushindani, Coastal Union watakuwa na kibarua kizito cha kusaka alama tatu muhimu ambazo zitawaokoa na kucheza mechi ya mchujo kubaki ligi kuu.
Aidha, pia Simba nao watataka kulinda heshima yao ya kufungwa mechi chache zaidi kwa msimu huu, kwani rekodi bado zinatambua hivyo pamoja na klabu ya Yanga ambao tayari wameshatwa ubingwa wa msimu huu.