Timu ya Yanga imefunika kwenye tuzo za msimu wa 2022/23 zilizotolewa kwenye ukumbi wa kituo cha soka cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) jijini Tanga.
Yanga imepata jumla ya tuzo 12 zikiwemo za mmoja mmoja na zile za kikosi bora.
Fiston Mayele pekee amechukuwa tuzo binafsi tatu ya Mfungaji Bora, Bao bora la msimu, Mchezaji Bora wa jumla wa msimu (MVP) pia yupo kwenye kikosi bora cha msimu.
Diarra ameondoka na tuzo mbili za kipa bora wa ASFC na Ligi Kuu huku Dickson Job akipata ya beki bora wakati Bakari Mwamnyeto akiwa mchezaji bora wa ASFC na wote wameingia kwenye kikosi bora.
Kocha Nabi amekuwa kocha bora, Clement Mzize ni mchezjai bora kijana chini ya miaka 20 anayecheza ligi kuu.
Simba ndiyo ilikuwa timu ya pili wachezaji wake kuchukuwa tuzo nyingi ikiongozwa na Saido Ntibazonkiza aliyebeba tatu ya mfungaji bora, Fair Play na kiungo bora pia yupo kwenye kikosi bora.
Wengine ni Henoc Inonga, Mohammed Hussein, Shomari Kapombe, Mzamiru Yassin, Clatous Chama ambao wote wameingia kwenye kikosi bora cha msimu.
Tuzo ya mchezaji bora chipukizi Ligi Kuu ni Lameck Lawi wa Coastal Union
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Championship ni Edward Songo wa JKT Tanzania
Tuzo ya Kamishina Bora wa Ligi Kuu imekwenda kwa Isack Munisi
Tuzo ya mwamuzi bora wa Ligi ya Wanawake (WPL) msimu wa 2022/23 imeenda kwa Ester Adalbert wakati mwamuzi msaidizi ni Glory Tesha.
Aidha mwamuzi bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23 amechukuwa Jonesia Rukyaa huku tuzo ya mwamuzi Msaidizi imechukuliwa na Frank Komba
Tuzo ya seti bora ya waamuzi imekwenda kwa Jonesia Rukyaa, Zawadi Yusuph, Athuman Rajabu na Ally Simba katika mechi ya Geita Gold na Dodoma Jiji
Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Wanawake 2022/23 ni Jentrix Shikangwa wa Simba Queens aliyefunga mabao 17
Kocha wa JKT Queens, Ally Ally amekuwa kocha bora wa Ligi Kuu ya Wanawake wakati mchezaji bora ni Donisia Minja
Chipukizi bora wa Ligi ya Wanawake ni Winfrida Charles wa Alliance Girls na kipa bora wa Ligi ya WPL ni Najat Abbas wa JKT Queens