Habari za Yanga leo
Habari za michezo

WAKATI YANGA WAKIMPA OFA YA MIL 40….KAIZER CHIEF WAMWEKEA NABI OFA YA MIL 100 KWA MWEZI…

admin June 14, 2023 3:25 pm

Kocha Nasreddine Nabi anaesakwa na klabu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika ya kusini, amewaambia Kaizer Chiefs anataka awe na timu yake ya Ufundi, Kocha Msaidizi, Kocha wa Makipa pamoja na mtaalamu wa video.

Kaizer wameweka dau la Sh 100 milioni kwa mwezi sawa na anazolipwa kocha wa sasa ambaye wanataka kumtoa baada ya kushindwa kutimiza malengo.

Taarifa kutoka Yanga zinasema kuwa mabosi wa klabu hiyo wakiongozwa na Injinia Hersi wako tayari kumlipa Nabi mshahara wa Milioni 40 kwa mwezi pamoja na marupurupu mengine, huku kukiwekwa kipengele cha mshahara huo kufikia mpaka Mil 50 endapo Yanga itafika fainal ya Klabu bingwa Afrika.

Hata hivyo upande wa Nabi unaoongozwa na mtoto wake, bado haujatoa jibu lolote kwa mabosi wa Yanga, ambapo inatzamiwa kuwa wakati wowote kutoka sasa wanaweza kufanya uamuzi mgumu.

Inafahamika kuwa makocha wote wa Yanga kwa sasa hawana mkataba na timu hiyo, huku baadhi ikitajwa wanataka kuondoka kwenda kupata changamoto mpya.

Inaelezwa kuwa Kocha msaidizi Cedrick Kaze ana ofa nono kutoka Singida Big Stars aambayo kwa sasainafahamika kama Singida Faunten gate FC.

Kocha wa makipa, Mbrazili Milivan naye anasemekama kuwa kwenye mawindo ya moja ya klabu za nnje ya nchi ambapo inatajwa dili hilo ni la kwenda kuwa kocha Mkuu.

Nabi amefanya vyema na Klabu ya Yanga akibeba Taji la Ligi Kuu, Azam Sports Federation huku akiifikisha Yanga hatua ya Fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

KUHUSU ISHU YA MKUDE NA NA KYOMBO KWENDA KUKIPIGA ULAYA…UKWELI WOTE HUU HAPA… HUYU HAPA MCHEZAJI MTZ ANAYETIKISA ULAYA …KOCHA TAIFA STARS KUMUITA KIKOSINI…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply