Home Habari za michezo BILA MSHAHARA WA MIL 35 KWA MWEZI MAYELE ANASEPA….YANGA WAKO TAYARI KUMPA...

BILA MSHAHARA WA MIL 35 KWA MWEZI MAYELE ANASEPA….YANGA WAKO TAYARI KUMPA MIL HIZI…

Habari za Yanga

Dau analotaka mshambuliaji hatari wa Yanga Fiston Mayele limewafanya mabosi wa Yanga kukuna kichwa kwani ni wazi kuwa ofa yake imekuwa kubwa kutokana na kiwango bora alichokionyesha katika misimu miwili mfululizo

Kwa sasa ni timu nyingi zimetajwa kumtaka mshambuliaji huyo mwenye tuzo ya ufungaji bora wa kombe la Shirikisho barani Afrika.

Imeelezwa kuwa timu moja kutoka Afrika Kusini imetuma ofa nono ikimtaka mshambuliaji huyo huku timu kadhaa za kutoka Mataifa ya kiarabu zikimtaka pia.

Pamoja na ofa nono ambazo zinamiminika Jangwani mabosi wa Yanga wanafanya juu chini kumbakisha mshambuliaji huyo.

Mayele aliporejea kutoka katika majukumu ya timu yake ya Taifa ya DR Congo aliitwa na mabosi wa Yanga na kukaa mezani kujadili kuhusiana na ofa zilizopo mezani lakini pia Yanga wakiwa wameweka ofa yao kwa mchezaji huyo aliyebakisha mkataba wa mwaka mmoja na Yanga.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga zinaeleza kuwa Yanga wametoa dau la mshahara wa dola za Marekani 12,000 (Tsh milioni 28) lakini Mayele amekataa akitaka kulipwa dola 15,000 (Tsh milioni 35) kwa mwezi.

Kama makubaliano yatafikiwa huenda siku ya Jumamosi kwenye mkutano mkuu, wanachama wakakutana na habari njema.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF KESHO KUTWA...MWAMNYETO AIWEKA YANGA KWENYE 'ENGO' NGUMU...

3 COMMENTS

  1. Si wamwache tupaye mayele mwingine. Vijijini kuna vipaji vikubwa sana lkn hamvioni na wala kuviendeleza. Mmebakia hapo Dar tu ndio wachezaji mnaowana. Tembeleeni timu za vijijini muone.

  2. Ana mkataba bado, kwahiyo kama ofa watume Yanga sio mayele. Baada ya Yanga kukubali aende aongee na club mpya personal benefits. Sawa na Mane kwenda Bayern Munich, Liverpool hawakutaka kumpa pesa zaidi .