Home Habari za michezo ‘UCHAWI’ WA KIBWANA SHOMARI WAMFANYA LOMALISA KUNYOOSHA MIKONO YANGA…

‘UCHAWI’ WA KIBWANA SHOMARI WAMFANYA LOMALISA KUNYOOSHA MIKONO YANGA…

SAFARI YA KIBWANA JANGWANI KIZUNGUMKUTI...LOMALISA AUNGUZA KIBANDA...SIJUI ITAKUAJE?

Zimevuja! Ndiyo utakavyoweza kusema ni baada ya sababu kujulikana za beki wa kushoto wa Yanga, Mkongomani Joyce Lomalisa Mutambala kuomba kuvunja mkataba.

Beki huyo mwenye uwezo mkubwa wakupiga krosi, wiki iliyopita ilielezwa kuandika barua ya kuomba mkataba wake wa mwaka ambao ameubakisha hapo uvunjwe.

Hiyo ikiwa siku chache zimebakia kabla ya usajili mkubwa wa msimu ujao kufunguliwa, ili timu shiriki za Ligi Kuu Bara zianze kufanya usajili wake.

Mmoja wa Mabosi wa Benchi la Ufundi la timu hiyo, amesema, sababu kubwa ya beki huyo kuomba kuvunja mkataba ni kutofurahia kuwekwa benchi na kiraka Kibwana Shomari anayemudu kucheza nafasi zote za beki wa pembeni.

Bosi huyo alisema kuwa Lomalisa anataka kuondoka hapo ili aende kwingine akapate nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza, lakini sio kuendelea kubakia hapo awekwe benchi na Kibwana.

Aliongeza kuwa uongozi umekubali kumuachia beki huyo aondoke, lakini kwa sharti la kuiita mezani klabu anayotaka kwenda kwa ajili ya kufanya mazungumzo rasmi.

“Uongozi tayari umemwambia kuwa upo tayari kumuachia aondoke hapo, lakini hiyo timu inayomtaka ije kwa uongozi wa Yanga kwa ajili ya mazungumzo.

“Kwani sababu yake inayomfanya avunje mkataba ya kitoto, kikubwa yeye kama anataka kucheza katika kikosi cha kwanza aongeze bidii ya kupambana uwanjani kila atakapopata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

SOMA NA HII  SAA CHACHE BAADA YA KUFUTWA KAZI..GOMES AANIKA YOTE YA SIMBA...AMTAJA MO DEWJI..AIKANA YANGA