Home Habari za michezo BAADA YA KUTEMWA YANGA BILA KUTARAJIA….’NINJA’ AKUMBUKA ALIYOAMBIWA NA ZLATAN…

BAADA YA KUTEMWA YANGA BILA KUTARAJIA….’NINJA’ AKUMBUKA ALIYOAMBIWA NA ZLATAN…

Habari za Michezo

Beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’, aliyepewa ‘Thank You’ na klabu ya Yanga baada ya kuwa nao kwa muda mrefu tangu 2017-2019 kisha kuondoka na kurudi hivi karibuni, amesema alijua mapema kwamba panmga lingemkuta kwa vile ndivyo maisha ya wachezaji walivyo popote duniani.

Ninja aliyewahi kukipiga nje ya nchi kabla ya kurejea 2020 kisha kutolewa kwa mkopo Dodoma Jiji na kurudia Jangwani msimu huu, amesema pamoja na kupigwa chini, lakini hadhani ndio itakuwa mwisho wa maisha yake ya soka, kwani anajipanga kupambana.

Yanga ilimsajili Ninja kwa mara ya kwanza 2017-2019 akitokea Taifa Jang’ombe, kisha akapata dili la kusajiliwa na MFK Vyskov (2019/2020) ambayo ilimtoa kwa mkopo La Galaxy ya Marekani, kisha akarejea tena Jangwani tangu hapo hakuwa na nafasi sana kikosini.

Ninja alisema changamoto alizokutana nazo haziwezi kuua ndoto zake, akitaja sababu kadha za kutokuwa kwenye kiwango bora tangu arejee kutoka nje ni majeruhi na baada ya kupona akaomba kwenda kwa mkopo Dodoma Jiji ambako alifanikiwa kucheza baadhi ya mechi.

“Maisha ya mpira yanahitaji ujasiri wa kupambana bila kukata tamaa, kwani ni kazi inayochezwa wazi, mchezaji unajajiwa na kile unachokionyesha uwanjani na siyo unachokipitia nje ya uwanja, majeraha yalinisumbua, lakini nashukuru klabu yangu ilinitibia kwa hivyo nipo fiti,” alisema Ninja.

“Ndio maana ilinipa mkataba wa mwaka mmoja, ambapo niliomba kwenda Dodoma kwa mkopo wa miezi sita, baada ya kurejea walichelewa kuchukua barua ya uhamisho, hivyo nikawa nakaa benchi, nje na hapo ningeonekana kwa baadhi ya mechi kwani kocha Nabi alikuwa anampa nafasi kila mchezaji kuonyesha uwezo wake.”

Aliwashukuru mashabiki wa Yanga kwa ushirikiano wao, tangu alipojiunga nao kwa mara ya kwanza, akiamini bado wataendelea kumuona akitumika klabu nyingine.

“Nakumbuka wakati nipo Marekani nilibahatika kuzungumza na Zlatan Ibrahimovic, aliwahi kuniambia mazingira ya aina yoyote yasije yakakukatisha tamaa, bali yatumie magumu kukufanya bora zaidi ya ulivyotazamwa jana,alinisisitiza mimi ni beki mzuri niamini kwenye kiwango na ndoto zangu siyo mtazamo wa mtu mwingine, tangu hapo sijawahi kukata tamaa tena.”

“Nitapata timu nitacheza na nitarejea kwenye makali yangu, bado nina muda mrefu wa kutumika kwa karia yangu, kikubwa ni bidii ya kunitoa sehemu moja kwenda nyingine.”

SOMA NA HII  EUROPA LEAGUE KUKUPATIA MAOKOTO LEO...