Habari za Michezo
Habari za michezo

BAADA YA KUKOSA DILI LA KAIZER CHIEF…NABI APAGAWA…..ASHINDWA KUZUNGUMZA…

admin June 28, 2023 8:44 pm

Klabu ya Kaizer Chiefs ya Afrika ya Kusini imemteua Molefi Ntseki kuwa kocha Mkuu wa klabu hiyo.

Kaizer Chiefs ilikuwa ikihusishwa kumtaka aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mtunisia Nsreddine Nabi.

Kwa utambulisho huo wa Molefi Ntseki kuwa Kocha wa Kaizer ni dhahiri kuwa Kocha Nabi bado yupo sokoni.

NABI APATWA KIGUGIMZI.

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amesema kuwa hawezi kuzungumzia sababu iliyokwamisha dili lake na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.

“Siwezi kutoa maelezo, kwa heshima ya Kaizer Chiefs. Sitaki kuzungumza kuhusu tatizo ni nini katika mazungumzo. Samahani kwa hilo,” Kocha, Nasreddine Nabi ameiambia #SundayTimes.

Nabi aliachana na Yanga baada ya kumalizika kwa msimu uliopita akiwa ameipa timu hiyo Ubingwa wa Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na Ngao ya Jamii, lakini akiwa ameifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kaizer Chiefs imekuwa ikitajwa muda mrefu kuwa inamhitaji kocha huyo, jana akihojiwa na gazeti maarufu la Afrika Kusini, The South Afrika alisema mazungumzo yanaendelea na ndani ya saa 48 wangekuwa wameshamalizana.

Kwa sasa Nabi yupo nchini Tunisia kulingana na vyanzo mbalimbali, wakati wakala wake yupo kwenye mazungumzo na Kaizer Chiefs kuhusu nafasi ya kocha mkuu.

WAKATI DILI LA KIBABAGE LIKISUBIRI SEKUNDE…MRITHI WA FEI TOTO YANGA HUYU HAPA… TAKWIMU ZINAONGEA….YANGA WAMEINGIZA PESA NYINGI KULIKO KLABU ZOTE ZA KENYA KWA UJUMLA WAKE…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply