Home Azam FC BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM…FEI TOTO AFUNGUKA ISHU YAKE NA RAIS SAMIA…AITAJA...

BAADA YA KUMALIZANA NA AZAM…FEI TOTO AFUNGUKA ISHU YAKE NA RAIS SAMIA…AITAJA YANGA…

Fei toto asaini Azam FC

Aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ amewashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho amefanya kazi katika klabu hiyo.

Fei Toto ametoa shukrani hizo mara baada ya kujiunga na Klabu ya Azam akitokea Yanga ambayo ameitumikia tangu mwaka 2018.

“Namshukuru kwa kufikia wakati huu, pia ninamshukuru sana Mhe. Rais Samia kwa kufanikisha kumaliza hili jambo hili, ninamuombea kwa Mungu ambariki na amjalie kila la kheri.

“Ninawashukuru mashabiki na viongozi wa Yanga kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja, ninawatakia kila la kheri. Mimi bado naipenda Yanga na mashabiki pia bado nawapenda, asanteni sana,” amesema Fei Toto.

Fei Toto amesaini mkataba wa miaka mitatu kuwatumikia Wauza Ukwaju wa Dar, baada ya kumaliza sakata lake la kimkataba na na Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

SOMA NA HII  AZIZI KI AFUNGUKA KILICHOMFELISHA MSIMU ULIOPITA,..... SASA MAMBO NI HIVI