Home Habari za michezo PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA…INJINIA HERSI ATAJA MFUMO WATAKAOTUMIA…

PANGA LA YANGA KUPITA NA MASTAA HAWA…INJINIA HERSI ATAJA MFUMO WATAKAOTUMIA…

Habari za Yanga leo

Wakiwa wameshatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23, Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said amebainisha namna watakavyopitisha panga kwa mastaa wa timu hiyo.

Ni ubingwa wa pili mfululizo wanasepa nao Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi raia wa Tunisia huku mchezo wake wa kwanza kupoteza msimu huu ikiwa ni dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Highland Estate.

Kuna mastaa ambao wanatajwa kupewa mkono wa asante ndani ya Yanga ikiwa ni pamoja na Dickson Ambundo, Crispin Ngushi, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Denis Nkane (kutolewa kwa mkopo) na Zawadi Mauya huku nyota wengine wakiwa kwenye mazungumzo ya kuboreshewa mikataba yao.

Injinia ameweka wazi kuwa kikubwa ambacho watakiangalia wakati wa kuachana na wachezaji wao ni mchango wao ndani ya timu pamoja na kuhitajika kwao kwenye timu nyingine.

“Tuna wachezaji wengi wazuri lakini wapo ambao tutawaacha hilo lipo wazi sio kwamba hawana uwezo hapana, ila kile ambacho wamekifanya kushindwa kuendana na kile tunachohitaji.

“Yanga inazidi kukua na kuwa kwenye ushindani mkubwa kitaifa na kimataifa lakini wapo wengine ambao tutaachana nao ikiwa watakuwa wanahitajika na timu nyingine na hapo ni lazima tuangalie namna bora ya kuwaacha hasa wale tunaowahitaji.

“Ikiwa tutashindwa kubaki na wale ambao tunawahitaji hakuna tatizo tuna falsafa ya kuwatafuta mbadala wao ili waendelee kuwa kwenye kikosi kwa kuwa maisha ni lazima yaendelee,” alisema.

SOMA NA HII  MKUDE AVUNJA UKIMYA SIMBA SC...AFUNGUKA A-Z KILICHONYUMA YA PAZIA..