Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA WAARABU…MASTAA WATULIZA PRESHA YANGA…MAYELE AONGOZA JAHAZI..

KUELEKEA MECHI YA MARUDIANO NA WAARABU…MASTAA WATULIZA PRESHA YANGA…MAYELE AONGOZA JAHAZI..

Yanga vs USMA

Wachezaji wa Yanga, wakiongozwa na Fiston Mayele na Kennedy Musonda, wamesema kuwa bado wana nafasi ya kushinda mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika watakapocheza nchini Algeria dhidi ya USM Alger.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Jumamosi ya wiki hii huko Algeria, baada ya mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kumalizika kwa Yanga kufungwa mabao 1-2 nyumbani.

Yanga wanahitaji ushindi wa uwiano wa mabao 2-0 ili wajihakikishie kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza nasi, mshambuliaji wa Yanga, Kennedy Musonda, alisema kuwa wana dakika nyingine 90 za ugenini za kuipambania Yanga na kuandika rekodi ya kubeba kombe hilo.

Musonda alisema kuwa kama wachezaji wameumizwa na matokeo hayo waliyoyapata nyumbani, ambayo yatawafanya waongezee bidii ya kuipambania timu na kupata matokeo ya ushindi.

“Tunafahamu mashabiki wa Yanga wameumizwa na matokeo ya kufungwa nyumbani, pia sisi tumeumia, hivyo wasikate tamaa, tuwaombe waendelee kutusapoti tutakapokwenda kurudana ugenini,” alisema Musonda.

Kinara wa mabao katika Kombe la Shirikisho Afrika, Fiston Mayele ambaye amepachika mabao saba, alisema kuwa mara baada ya mchezo huo wanakwenda kufanya kikao, kikubwa ni kukumbushana kwenda kulipa kisasi Algeria.

“Mashabiki wetu wa Yanga wasikate tamaa kwa kupoteza mchezo wa kwanza wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kwani bado tunayo nafasi ya kushinda mchezo wa marudiano.

“Haitakuwa kazi nyepesi kwetu, lakini kwa nguvu za Mungu, ninaamini tunakwenda kupata matokeo mazuri ya ushindi ugenini. Kwani kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huo,” alisema Mayele.

SOMA NA HII  UCHAGUZI WAITIKISA SIMBA SC...WANACHAMA WAMCHAGUA MWENYEKITI....MATABAKA YAZALIWA