Home Uncategorized MTUPIAJI POLISI TANZANIA AWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

MTUPIAJI POLISI TANZANIA AWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA


SIXTUS Sabilo, mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa kwa sasa ni muhimu kwa kila mmoja kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kuwa salama.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sabilo amesema kuwa amejichimbia zake Bunda, Mara huku akichukua tahadhari dhidi ya Corona pamoja na kuwa balozi kwa familia na jamii pia.

“Baada ya ligi kusimamishwa kambi ilivunjwa nami nikaibukia nyumbani Bunda, ninachukua tahadhari ya Virusi vya Corona na ninashauri wote tuungane katika hili.

“Ni janga la dunia na kila mmoja anapaswa awe makini ili kuwa salama kwani afya ni muhimu kuliko mpira huwezi kucheza iwapo hauna afya,” amesema.

Kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa, Sabilo alitupia mabao saba.

SOMA NA HII  SUALA LA OKWI LAIBUKA UPYA SIMBA, KIGOGO AFUNGUKA JUU MATUMIZI YA FEDHA ZAKE