Home Habari za michezo PAMOJA NA KUAMBULIA MEDALI JANA…RAIS SAMIA AENDELEA KUFANYA ‘MAJAMBOZI’ KWA YANGA…HILI HAPA...

PAMOJA NA KUAMBULIA MEDALI JANA…RAIS SAMIA AENDELEA KUFANYA ‘MAJAMBOZI’ KWA YANGA…HILI HAPA LINGINE…

Habari za Yanga

Katika kutambua mchango wa klabu ya Yanga katika michuano ya kimataifa, Rais Samia Suluhu Hassan kesho Jumatatu Juni 5, 2023 ameialika klabu hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya chakula cha jioni.

Rais Samia amesema pamoja na timu hiyo kutotwaa ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika (CAFCC), lakini imeipa heshima Tanzania pia amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo ambao pia ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara.

Yanga iliichapa USM Alger bao 1-0 katika fainali ya pili ugenini nchini Algeria usiku wa kuamkia leo Juni 4, 2023, hata hivyo imeshindwa kutwaa ubingwa kwa wenyeji kutakata kwa matokeo ya awali ya mabao 2-1 iliyopata kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam katika fainali ya kwanza iliyofanyika Mei 28, 2023.

Baada ya matokeo hayo, jana Rais Samia kwenye mtandao wake wa kijamii wa Twita aliipongeza Yanga kwa hitimisho la fainali hiyo.

“Historia mliyoandika katika safari yenu ya michuano hii mikubwa na ya heshima kwa taifa letu, nawatakiwa heri katika mipango yenu ya siku zijazo,” aliandika Rais Samia.

Mapema leo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais pia ameialika timu kwa chakula cha jioni Ikulu, Jijini Dar es Salaam kesho Jumatatu kwa lengo kuipongeza kwa kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Amesema ameipongeza Yanga kwa kucheza vizuri katika mchezo wa pili wa fainali kwa kuwafunga wenyeji bao 1-0 na kuwa na matokeo ya jumla ya mabao 2-2 japokuwa hawakufanikiwa kutwaa ubingwa.

“Pamoja na kutotwaa ubingwa, Rais Samia anatambua kuwa Yanga wameipa heshima kubwa Tanzania na anawapongeza wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo ambao ni Mabingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara,” iilieleza taarifa ya Msigwa.

SOMA NA HII  KISA SIMBA...YANGA WAWEKEWA BILIONI MOJA...PABLO APIGA HESABU KALI..YANGA, AZAM ZAINGILIA USAJILI...