Home Habari za michezo KUHUSU UJIO WA MAKABI BONGO….TAARIFA MPYA HII HAPA KUTOKA SIMBA SC…

KUHUSU UJIO WA MAKABI BONGO….TAARIFA MPYA HII HAPA KUTOKA SIMBA SC…

Habari za Simba

Klabu ya Simba SC inatajwa kutaka kumsajili Kiungo Mshambulizji kutoka DR Congo na klabu ya Al Hilal Omdurman ya Sudan, Makabi Lilepo kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chake kuelekea michuano ya Supa Ligi, Ligi Kuu Tanzania Bara na Klabu Bingwa Barani Afrika.

Inaelezwa kuwa uongozi wa klabu hiyo umeanza mchakato huo na wanataka nyota huyo awemo kwenye maandalizi ya msimu mpya waliopanga kuanza mwishoni mwa mwezi ujao.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa klabu hiyo Ahmed Ally alipoulizwa kuhusu usajili wa Kiungo huyo, amesema wapo wachezaji ambao kocha wa timu hiyo amependekeza kusajiliwa kuimarisha timu hiyo.

“Siwezi kusema nani na nani ambao wamependekezwa kusajiliwa, lakini ni wachezaji wenye kariba ya Lilepo,” amesema Ahmed na kuongeza,

“Ni ngumu kutaja mchezaji mmoja mmoja tunahitaji wachezaji wengi wenye kariba na aina ya nyota kama Lilepo, mwenye sifa ya kuitumikia Simba na kufikia malengo yetu ya kurejesha mataji tuliyoyapoteza na kutimiza malengo yetu ya kucheza nusu fainali ya klabu bingwa Afrika,” amesema Ahmed

Amesema suala la usajili mashabiki wa timu hiyo waondoe hofu na watajulishwa kila mchezaji watakayekuwa wamemalizana naye.

“Kwa sasa bado ni tetesi, tunaweza kusema hivyo, mashabiki wetu wasiwe na hofu, uongozi utakapokuwa umekamilisha kila dili la mchezaji basi tutawatangazia mashabiki wetu, Simba tunafanya mambo yetu kwa umakini mkubwa,” amesema Ahmed

Amesema kwenye suala hilo la usajili uongozi unawasiliana kwa karibu na kocha wao Robertinho ambaye kwa sasa yupo mapumzikoni kwao Brazil.

Jana Alhamis (Juni 15) Simba SC ilitangaza kuachana na Kocha wa makipa Chlouha Zakaria raia wa Morocco ambaye alitanguliwa na makocha wa viungo raia wa Afrika Kusini Kelvin Mandla Ndlomo na Fareed Cassiem ambao wamepewa mkono wa kwa heri.

SOMA NA HII  BAADA YA KUKIONA KIKOSI CHA SIMBA...PABLO 'AWAKATA MAINI' WANAOTARAJIA MAFANIKIO YA HARAKAHARA ...