Home Habari za michezo FT: HAYA HAPA MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO….MAYELE NA NTIBAZONKIZA WAGAWANA...

FT: HAYA HAPA MATOKEO YOTE YA MECHI ZA LEO….MAYELE NA NTIBAZONKIZA WAGAWANA TUZO…

Habari za Yanga leo

Fiston Mayele wa Yanga na Saido Ntibazonkiza wa Simba wamegawana tuzo ya mfungaji bora wa Ligi kuu ya NBC iliyotamatika mapema hii leo.

Mastaa hao kwa nyakati tofauti wamezifungia magoli timu zao, huku Saidoo akifunga magoli 2 yaliyomfanya kumfikia Mayele ambaye naye alifunga goli 1 hivi leo kwenye mechi dhidi ya Tanzania Prisons.

UBAO wa Uwanja wa Uhuru unasoma Simba 3-1 Coastal Union ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Saido Ntibanzokiza alifunga bao la kuweka usawa dakika ya 13 akisawazisha bao la Coastal Union waliopachika bao la kuongoza kwa pigo la penalti dakika ya 7 kupitia kwa Amza Moboubarack.

John Bocco kipindi cha pili amepachika bao la pili kwa Simba dakika ya 56 na kamba ya tatu imepachikwa na Saido Ntibanzokiza anayefikisha mabao 17 kwenye ligi.

Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili ikiwa ni wa mwisho kwa timu zote ndani ya Bongo na mabingwa ni Yanga ambao wanamaliza na Tanzania Prisons ya Mbeya.

Aidha katika hatua nyingine, huko Mbeya FISTON Mayele anachojua ni kufunga mengine weka kando kambani ni mabao 17 kwenye Ligi Kuu Bara.

Ubao wa Uwanja wa Sokoine unasoma Tanzania Prisons 0-2 Yanga ikiwa ni mchezo wa ligi.

Bao hilo amepachika dakika ya 33 akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Sure Boy.

Yanga leo wamekabidhiwa ubingwa wao wakiwa ardhi ya Mbeya, Uwanja wa Sokoine.

Mayele anaongoza kwa mabao ndani ya Yanga akiwa ni namba moja anapambania kutwaa tuzo ya ufungaji bora.

Goli la pili kwa Upande wa Yanga limefungwa katika Dakika za nyongeza na kiungo Yannick Bangala.

Matokeo mengine ni :-

Mbeya City 0-1 KMC FC

Mtibwa Sugar 3-1 Geita Gold FC

Ihefu 2-0 Kagera Sugar FC

Namungo 1-1Singida BS FC

Ruvu Shooting 0-1 Dodoma Jiji FC

Azam FC 8-0 Polisi Tanzania FC

SOMA NA HII  NABI:- YANGA HATUTARUDIA MAKOSA KWA MAZEMBE...