Home Habari za michezo LILE DILI LA STRAIKA MCAMEROON KUTUA SIMBA ‘UPDATE’ HII HAPA….MBRAZILI ALETA KOCHA...

LILE DILI LA STRAIKA MCAMEROON KUTUA SIMBA ‘UPDATE’ HII HAPA….MBRAZILI ALETA KOCHA MSAIDIZI MPYA..

Tetesi za Usajili Simba

HAKUNA utani. Mabosi wa Simba SC, wamekamilisha usajili wa majembe mawili kwa mpigo, akiwemo mfungaji bora wa Ligi Kuu Rwanda, Leandre Essomba Onana raia wa Cameroon ambaye unaambiwa alifichwa jijini hapa (Dar) kwa siku tatu ili kukamilisha taratibu za usajili wake ikiwemo kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa taarifa mfungaji bora huyo aliyepachika mabao 16 huko Rwanda msimu huu, alifanyiwa vipimo vya afya juzi, huku asubuhi ya jana akisaini mkataba wa miaka miwili kukipiga kwa wekundu hao wa Msimbazi sambamba na kocha wa viungo ambaye naye ametokea Rwanda, Hategekimana Corneille lakini rekodi zinaonyesha aliwahi kufanya kazi na kocha wa sasa wa Simba Robert Olivier Robertinho wakiwa Rayon Sports.

Onana anatazamwa kama mbadala ya Jean Baleke ambaye mkataba wake wa mkopo kukipiga Msimbazi umemalizika huku Corneille akibebeshwa mikoba ya Kelvin Mandla ambaye amrejea kwao Afrika Kusini baada ya mkataba wake kumalizika.

Mmoja wa watu ambao wamekuwa sehemu ya mazungumzo kufanikisha dili la Onana alisema, “Mambo yameenda vizuri kama ambavyo ilipangwa na amesaini mkataba wa miaka miwili, na Wanasimba wategemee kumuona (Onana), akiwatumikia msimu ujao, amekuwa na wakati mzuri Rwanda, na kwa bahati nzuri ligi ya Tanzania alikuwa akiifuatilia.”

Mcameroon huyo alitua Kigali Septemba 2021 kama sehemu ya takriban wachezaji 50 walioenda Rayon Sports kwa majaribio katika dirisha hilo la uhamisho.

Kabla ya kwenda Rayon Sports kwa majaribio, mchezaji huyo alikuwa amejizolea umaarufu mkubwa nchini kwao akiwa na klabu ya Ending Sport FC, inayojulikana nchini Cameroon kwa kukuza vipaji vya vijana.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa na Rayon, fowadi huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao kumi ya ligi lakini kiwango chake kizuri katika msimu wa 2022/23 kilishuhudia idadi ya mabao yake ikiimarika, akifunga mabao 16 na kutoa asisti tano kwenye michezo 23 ya ligi na mabao manane ya Kombe la Amani.

Mabao yake yalikuwa muhimu kwa ushindi wa kwanza wa Blues wa Kombe la Amani ndani ya miaka saba kando na kumaliza wa tatu kwenye ligi kwa pointi 61, mbili nyuma ya mabingwa APR FC.

Rayon Sports sasa wanajiandaa kwa maisha bila Onana kwa kusaka mbadala sahihi ambaye anaweza kuleta matokeo wakati wa kampeni yao ya Kombe la Shirikisho la CAF 2023/24 na pia kumenyana na APR msimu wa 2023/24.

Onana ameondoka Rwanda akiwa na tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Rayon. Pia akitarajiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda 2022/23.

SOMA NA HII  CHUKUA HII YA MOTO MOTO....VICTORIEN ADEBAYOR NI MWEKUNDU RASMI...MKATABA WAKE HUU HAPA...