Home Cecafa Cup KOMBE LA KAGAME MIKONONI MWA EXPRESS YA UGANDA

KOMBE LA KAGAME MIKONONI MWA EXPRESS YA UGANDA


 TIMU ya Express ya Uganda imetwaa taji la Kagame Cup 2021 kwenye ardhi ya Tanzania baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Big Bullets ya Malawi kwenye mchezo wa fainali uliochezwa jana Agosti 14 Uwanja wa Mkapa.

Ushindi huo unaifanya iweze kupokea kijiti kutoka kwa KCCA ya Uganda ambao walikuwa ni mabingwa watetezi lakini walikwama kutinga hatua ya nusu fainali msimu huu.

Kwa upande wa wawakilishi wa Tanzania, KMKM wamekuwa ni washindi wa tatu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.

Ilikuwa ni timu tatu kutoka Tanzania zinashiriki mashindano hayo ikiwa ni Azam FC, KMKM kutoka visiwani Zanzibar na Yanga.

Yanga iliishia hatua ya makundi huku Azam FC na KMKM zikiishia hatua ya nusu fainali katika mashindano hayo. 

SOMA NA HII  YANGA KAZINI LEO KAGAME CUP, YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA