Home Habari za michezo BAADA YA KUTEMWA JANA ..AMBUNDO ASHINDWA KUJIZUIA…AANIKA MAMBO YOTE YA YANGA WAZI…

BAADA YA KUTEMWA JANA ..AMBUNDO ASHINDWA KUJIZUIA…AANIKA MAMBO YOTE YA YANGA WAZI…

Habari za Yanga leo

Yanga ikiendeleza ‘Thank You’ jana imeachana na winga Dickson Ambundo ikiwa inafumua kikosi kwa ajili ya msimu ujao.

Ambundo amewaaga Wananchi na kwa kutoa ujumbe wenye hisia kupitia akaunti yake ya Instagram akiandika;

“Moja kati ya nyumba bora sana, nyumba yenye upendo, furaha, matumaini na umoja wa hali ya juu, nyumba ya mafunzo yanayotoa mwanga mzuri kwenye safari ya maisha, kwa huzuni leo nawaaga wenzangu kwenye nyumba lakini moyo wangu umejawa na shukrani za dhati kabisa kwa wenye nyumba kuanzia uongozi bora kabisa chini ya Rais Hersi Said, benchi la ufundi chini ya Nasreddine Nabi, wachezaji wenzangu na wananchi wote kwa ujumla.

Mungu aendelee kuwabariki kuleta mafanikio zaidi katika safari yenu. Siku moja tutaonana tena nyumbani. Daima Mbele, nyuma mwiko,”

Habari za ndani zinasema tayari uongozi wa Dodoma Jiji umeanza kufanya mazungumzo na mchezaji huyo na kama mambo yakienda sawa basi msimu ujao atakuwa sehemu ya kikosi chao.

“Ni mchezaji mzuri sana, ndani ya kikosi cha Yanga kuna ushindani mkali hivyo kutocheza mara kwa mara kunamfanya aonekane ameshuka kiwango,” alisema mmoja wa kiongozi wa Dodoma Jiji.

Winga huyo ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo wa kucheza pande zote mbili kushoto na kulia uwanjani na kufanya umuhimu wao uonekane.

SOMA NA HII  LEO TENA.....MPAPATUKO WA LIGI YA NBC KUTIMUA VUMBI....RATIBA KAMILI HII HAPA....'MZUNGUU' WA SIMBA ATATOA GUNDU..?