Home Habari za michezo WAKATI MITANDAONI TETESI NI NYINGI…MABOSI SIMBA ‘WAKUNJANA MASHATI’…ISHU YA CAF YATAJWA..

WAKATI MITANDAONI TETESI NI NYINGI…MABOSI SIMBA ‘WAKUNJANA MASHATI’…ISHU YA CAF YATAJWA..

Habari za Simba SC

SIMBA wamejifungia kwenye hoteli moja ya jiji la Dar es Salaam kwa siku mbili, huku ubishani ukiwa mkubwa kuhusu mambo mawili.

Simba haijafanikiwa kutwaa ubingwa wowote msimu huu, lakini pia haikufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuishia hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mabosi wa timu hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Salim Abdallah ‘Try Again’ walianza vikao hivyo Ijumaa iliyopita kwa makubaliano kuwa kitakuwa cha siku moja, lakini kutokana na uzito wa hoja, walijikuta wakikaa kwa siku mbili na bado hawajamaliza.

Moja ya jambo ambalo Simba walijadili ni usajili kwa ajili ya michuano mipya ya Super Cup, lakini pia maandalizi ya kambi yao ya kabla ya msimu ujao kuanza.

Chanzo cha ndani kutoka ndani ya kikao hicho kinasema kuwa mabosi walibishana kuhusu aina ya usajili waliokuwa wakifanya, huku wakihusisha na vigogo kadhaa ambao watapambana nao kwenye Super Cup, kama Mamelodi Sundowns, Al Ahly na hata Wydad Casablanca.

“Tulijadili mambo mengi, lakini kubwa ni usajili kwa ajili ya mashindano ya Super Cup yanayoanza mwezi Agosti, hapa tulijadili mambo mengi lakini ugumu pia wa ratiba.

“Wajumbe walikuwa wakali kwa kuwa wanaamini mashindano haya ndiyo yataonyesha tuna kikosi cha namna gani kwa kuwa tunakwenda kupambana na vigogo wa Afrika, huku hakuna timu ndogo ndiyo maana unaona tumekaa muda mrefu,” alisema bosi huyo na kuongeza:

“Hata hivyo, ishu ya kambi naona tuliimaliza kwa kuwa wengi walipendekeza timu iende Uturuki baadaye mwezi ujao, bado tutalijadili lakini hili limeshapita labda kuwe na ishu nyingine.”

Chanzo hicho kilisema majina kadhaa yametajwa kwenye usajili, lakini utaratibu maalumu wa kuwatangaza umeshawekwa sawa.

“Kuna wachezaji nafikiri ni watatu tayari tumeshawasajili, klabu inasubiri dirisha lifunguliwe ndiyo watangazwe rasmi kuna utaratibu umewekwa, wengine tunaendelea kubishana ili kuhakikisha tunapata wale bora kwa kuwa fedha za Super Cup zipo hivyo hakuna shida sana.”

Timu nane zinatarajiwa kushiriki mashindano ya Super Cup ambayo ni mapya na yatachezwa kwa mfumo wa nyumbani na ugenini ambazo ni Petro de Luanda (Angola), Mazembe (DR Congo), Mamelodi (Afrika Kusini) Horoya (Guinea), Wydad Atheltic Club (Morocco), Al Ahly (Misri) Simba SC (Tanzania) na Esperance de Tunis (Tunisia).

SOMA NA HII  SIMBA WAKIINGIA NA 'PLAN' HIZI MBELE YA AL AHLY.....MECHI INAISHIA HAPA HAPA BONGO...