Home news SENZO AUKATAA UBINGWA KWA YANGA….AWANYOOSHEA KIDOLE WACHEZAJI..NABI AKOLEZA ‘PILIPILI’

SENZO AUKATAA UBINGWA KWA YANGA….AWANYOOSHEA KIDOLE WACHEZAJI..NABI AKOLEZA ‘PILIPILI’

 


KAIMU ofisa mtendaji mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa amesema licha ya timu kupata matokeo mazuri, amewataka wachezaji wasibweteke kwani vita ya ubingwa sio ndogo.

Senzo alisema kinachotakiwa kufanyika ni kuendelea kushinda mfululizo na kupata pointi nyingi ambazo zitawasaidia mwishoni mwa msimu watakapoanza kuhesabu pointi walizonazo.

“Tumeshinda ngao msimu huu, kwa hiyo kilichobaki ni kuweka nguvu katika kila mchezo kuhakikisha tunafanya vizuri. Ni mapema kusema tutachukua ubingwa ikiwa kama hatushindi,” alisema Senzo.

Kigogo huyo alisema Ligi Kuu ni kama mbio za marathon na muda wote unatakiwa uwe vizuri, lakini yeye kama kiongozi wa juu pamoja na benchi la ufundi na wachezaji wanaahidi utakuwa msimu bora kwao.

Naye kocha Nassredine Nabi alisema: “Niliomba miezi mitatu wakati natoka Morocco na sasa ni miezi miwili tu timu yangu ipo katika asilimia 50. Ikifika miezi mitatu basi tutakuwa katika asilimia 100.”

“Nampongeza sana mwalimu wangu wa viungo kwa kuzidi kuwafanya wachezaji kuwa vizuri. Nadhani kila mmoja ameona namna ambavyo timu yetu katika mechi na Azam ilivyocheza, ingeweza kucheza zaidi ya dakika walizocheza.”

SOMA NA HII  MHILU..MKUDE WAANZA KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA NAMUNGO..KIKOSI KAMILI HIKI HAPA...