Home Habari za michezo MAYELE:- MOROCCO SAWA…, ILA TANZANIA MHHHH…..

MAYELE:- MOROCCO SAWA…, ILA TANZANIA MHHHH…..

Habari za Michezo leo

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Pyramid FC ya Misri na timu ya taifa ya DR Congo, Fiston Mayele amesema mchezo wao dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ hautakuwa rahisi na wanauchukulia kama fainali.

Mayele amefunguka hayo muda mchache baada ya timu yake kuambulia sare ya bao 1-1 dhidi ya Morocco huku akikiri alama mbili walizovuna kwenye mechi mbili sio salama kwao.

“Tumekutana na Morocco ni wazuri kwa sababu wana wachezaji wengi wazuri, tumepambana na kuambulia pointi moja, sio haba kwetu sasa tunaenda kumaliza dhidi ya Tanzania utakuwa mchezo mzuri, kwetu ni kama fainali;

“Nitakutana na wachezaji wengi ambao nawafahamu, nimecheza nao, naamini kila mmoja atapambana kuhakikisha tunavuka hatua inayofuata,” alisema Mayele ambaye alicheza kwa mafanikio Ligi Kuu Bara akimaliza msimu akiwa mfungaji bora na mabao 17.

Mayele alisema wataingia kwa kuwaheshimu wapinzani wao huku wakiwa wamejiandaa kupambania taifa lao tayari kwa ajili ya kuhakikisha wanatinga 16 bora.

DR Congo ipo kundi F sambamba na Morocco ambao wanaongoza kundi, Zambia nafasi ya tatu, Tanzania. Imekusanya pointi mbili kutokana na sare mbili ilizozipata dhidi ya Zambia na Morocco.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPOKEA KICHAPO CHA 'HAJA' JANA...KOCHA USGN KAONA ISIWE TABU...KAFUNGUKA HAYA ....