Home Habari za michezo WAKATI DILI LA KIBABAGE LIKISUBIRI SEKUNDE…MRITHI WA FEI TOTO YANGA HUYU HAPA…

WAKATI DILI LA KIBABAGE LIKISUBIRI SEKUNDE…MRITHI WA FEI TOTO YANGA HUYU HAPA…

Tetesi za Usajili Yanga

Mashabiki wa Yanga walishamsahau kiungo wao Feisal Salum ‘Fei Toto’ na sasa wajiandae kumuona mbadala wake mpya katika timu hiyo, Yusuf Kagoma aliyefikia muafaka mzuri na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Kiungo huyo alikuwa akitajwa Simba kabla ya Yanga kuanza mazungumzo na kukamilisha dili lake haraka ili aje kucheza nafasi ya kiungo ya ukabaji katika msimu ujao.

Yanga imepanga kukifanyia kikosi chake ili kifanye vema katika msimu ujao ambao timu hiyo, ina kibarua cha kutetea mataji yake mawili Ligi Kuu Bara, Kombe la FA na kufika hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kwa mujibu wa mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Jumamosi, kuwa dili hilo limekamilika kwa asilimia kubwa kati menejimenti ya mchezaji na uongozi wa Yanga.

Bosi huyo alisema kuwa dili hili limekamilishwa haraka kwa ajili ya kuiboresha safu ya kiungo ambayo alikuwa akihitajika kiungo mkabaji mzawa anayemudu kucheza viwanja vya aina yote.

Aliongeza kuwa kiungo amechaguliwa yeye kusajiliwa kati ya viungo wazawa kutokana na kucheza kwa kiwango bora katika msimu uliopita, hivyo amestaili kusajiliwa na Yanga.

“Viungo wakabaji tunao wengi, lakini benchi la ufundi lilimuhitaji Kagoma kutokana na kumudu vema nafasi hiyo ya kiungo ukabaji namba 6.

“Ni kiungo anayeweza kuzuia na kupunguza mashambulizi golini kwake, hivyo uwepo wake kutaimarisha kikosi chetu kama unavyofahamu msimu ujao tutacheza mashindano mengi, hivyo ni lazima tuwe na kikosi kipana.

“Tutahakikisha tunafanya usajili katika kila sehemu zaidi ya mchezaji mmoja ili tufanikishe malengo yetu katika msimu ujao, tayari tumemalizna na baadhi ya wachezaji wapya hivi karibuni tutaweka wazi,” alisema Bosi huyo.

Yanga kwa kupitia Rais wa timu hiyo, Injinia Hersi Said hivi karibuni alizungumzia usajili kwa kusema: “Tumepanga kumsajili mchezaji yuleambaye yupo katika ripoti ya usajili, pesa sio tatizo kwetu Yanga tumepanga kufanya vema msimu ujao.”

KIBABAGE NI SUALA LA MUDA TU.

Klabu ya Yanga imeripotiwa kufikia makubaliano ya masharti binafsi na mlinzi wa kushoto wa Singida Fontaine Gate FC, Nickson Kibabage kwa ajili ya kuvaa uzi wa kijani na njano msimu ujao.

Yanga SC inaendelea na majadiliano na Wakulima hao wa Alizeti juu ya dau la uhamisho. Kibabage bado ana mkataba na Singida Fontaine Gate FC.

Inaelezwa Kibabage alikuwa pendekezo la kocha Nasreddine Nabi aliyeondoka klabuni hapo hivyo Wananchi wameamua kulitekeleza baada ya kuona anafaa kuvaa uzi wa Wanajangwani.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE