Home news KILE KICHAPO CHA GOLI 7-0 KUTOKA SIMBA CHAZIDI KUMVURUGA MKWASA…AENDELEA KUMUOTA SONSO…

KILE KICHAPO CHA GOLI 7-0 KUTOKA SIMBA CHAZIDI KUMVURUGA MKWASA…AENDELEA KUMUOTA SONSO…


L ICHA ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Prisons, Kocha Mkuu Ruvu Shooting, Charles Mkwasa, amefunguka kuwa bado wachezaji wake hawajakaa sawa kisaikolojia kutokana na msiba wa aliyekuwa beki wa timu hiyo, Ally Mtoni maarufu Sonso.

Ruvu Shooting ilipoteza kwa mabao 7-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa raundi ya tano ya Kombe la Shirikisho la Azam uliopigwa Jumatano iliyopita, kabla ya juzi Jumapili kuibuka na ushindi dhidi ya Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Dimba la Sokoine, Mbeya.

Februari 11, mwaka huu, Ruvu Shooting ilipata pigo baada ya Sonso aliyekuwa akicheza beki wa kati kikosini hapo, kufariki kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya mguu.

Akinukuliwa na gazeti la  Spoti Xtra, Mkwasa alifunguka kwamba: “Tumepata matokeo chanya ambayo tulikuwa tunayatarajia, ni jambo jema lakini bado vijana wangu hawapo sawa kisaikolojia kutokana na msiba mzito uliotukuta wa kumpoteza mchezaji wetu Sonso. “Itawachukua muda kidogo kurudi kwenye hali ya kawaida ukizingatia hata mchezaji ambaye alikuwa analala naye chumba kimoja bado hajawa sawa kisaikolojia na hajaungana na wenzake.

Tunarudi nyumbani kuendelea na maandalizi kwa ajili ya michezo yetu inayofuata, hatupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi, hivyo tunahitaji kupambana ili tuweze kujinasua kwenye nafasi za chini.” Ruvu Shooting inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 15 baada ya kushuka dimbani katika mechi 15 wakishinda nne, sare tatu na kupoteza nane.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMKATAA AWALI KUWA HAENDANI NA FALSAFA YAKE....HATIMAYE ZORAN ANYOOSHA MIKONO JUU KWA CHAMA....