Home news PABLO ALIA WACHEZAJI WA SIMBA KUKOSA PUMZI NIGER…ADAI HALI YA HEWA NI...

PABLO ALIA WACHEZAJI WA SIMBA KUKOSA PUMZI NIGER…ADAI HALI YA HEWA NI TATIZO..


KOCHA Mkuu wa Simba, Pablo Franco Martin raia wa Hispania, amefunguka kuwa wachezaji wake walikutana na hali ngumu wakiwa Niger kiasi cha kushindwa kupumua vizuri kutokana na hali mbaya ya hewa.

Pablo aliweka wazi kuwa, haikuwa kazi rahisi kwao kupata pointi moja mbele  ya US Gendarmarie kwani kila kitu kwao hakikuwa rafiki, mbali na hali mbaya ya uwanja kwenye sehemu ya kuchezea, hata hali ya hewa ilikuwa tatizo.

“Wachezaji wangu wanapaswa kupongezwa sana kwa kile walichopata tukiwa Niger, kulikuwa na mazingira magumu sana, hali ya hewa ilikuwa mbaya sana kiasi cha wachezaji kupumua kwa tabu.

“Uwanja hasa eneo la kuchezea hapakuwa rafiki hata kidogo, kila kitu kilikuwa kigumu. Lakini wachezaji waliungana na kuipambania timu yao.”

Simba walipata alama moja ugenini wikiendi iliyopita na kufikisha nne kileleni mwa msimamo wa Kundi D. Februari 27 watashuka dimbani kucheza na RS Berkane ikiwa ni mchezo wao wa tatu hatua ya makundi.

SOMA NA HII  ZA NDAAANIIIII.....YANGA WAMRUDIA MAKABI LILEPO 'USIKU USIKU'.....ISHU NZIMA IMEKAA HIVI...