Home Habari za michezo ZA NDAAANIIIII…..YANGA WAMRUDIA MAKABI LILEPO ‘USIKU USIKU’…..ISHU NZIMA IMEKAA HIVI…

ZA NDAAANIIIII…..YANGA WAMRUDIA MAKABI LILEPO ‘USIKU USIKU’…..ISHU NZIMA IMEKAA HIVI…

Tetesi za Usajili Bongo

MABOSI wa Yanga, wameiangalia safu yao ya ushambuliaji katika michezo ya Ngao ya Jamii, fasta wakachukua uamuzi wa kumrudia mshambuliaji wa Al Hilal ya Sudan, Mkongomani, Makabi Lilepo.

Awali Yanga ilifanya mazungumzo na mshambuliaji huyo, ambaye walitaka kumsajili katika usajili huu ili kuchukua nafasi ya Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika, Fiston Mayele aliyetimkia Pyramids FC ya Misri.

Yanga ilishindwa kufikia muafaka mzuri na uongozi wa Al Hilal kwa ajili ya kumsajili Lilepo, kabla ya kuhamishia nguvu kwa Mghana, Hafizi Konkoni aliyetambulisha hivi karibuni.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, amesema kuwa, uongozi wa timu hiyo umekubali kuvunja benki na kumtengea Lilepo kitita kikubwa cha dau la usajili ili akubali kusaini mkataba wa miaka miwili aliowekewa mezani.

Bosi huyo alisema mshambuliaji huyo hivi sasa ameondoka katika kambi ya Al Hilal kama sehemu ya kushinikiza aruhusiwe kuondoka hapo kabla ya dirisha la usajili kufungwa Agosti 31, mwaka huu.

Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo yupo katika mazungumzo na mabosi hao wa Yanga, na kama yakienda vizuri, basi atasaini.

“Uongozi umeangalia kikosi chetu katika mashindano ya Ngao ya Jamii na kugundua upungufu mkubwa katika safu ya ushambuliaji ambayo ni lazima wampate mshambuliaji wa kiwango kikubwa zaidi ya hao waliokuwepo sasa.

“Lilepo ni kati ya washambuliaji watakaosajiliwa kabla ya dirisha kufungwa msimu huu, kwani ni mchezaji aliyekuwepo katika mazungumzo mazuri na uongozi baada ya yeye mwenyewe kuhitaji kuja Yanga.

“Tayari mshambuliaji huyo ameondoka kambini huko Al Hilal akishinikiza kuondoka, hivi sasa yupo katika mazungumzo mazuri na vongozi wake na kama yakienda vizuri, basi huenda akasaini Yanga kabla usajili haujafungwa,” alisema bosi huyo.

Makamu wa Rais wa Yanga, Arafat Haji, hivi karibuni katika Wiki ya Wananchi, alizungumzia usajili na kusema kuwa: “Bado hatujafunga usajili wetu wa msimu huu, hivyo tunaweza kuongeza wachezaji mmoja hadi wawili kabla ya dirisha kufungwa.”

SOMA NA HII  EDO KUMWEMBE - KITUO KINACHOFUATA KWA SIMBA NI KWA WAKUBWA WENZAO...TUTAONA UKUBWA WAO..