Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi Bw.Francis Tu alisema, “Infinix ni brand inayotambulika duniani kote, leo tuna furaha kutangaza Infinix NOTE 30 Series, tumebuni series hii ya NOTE kwa lengo la kuwapa watumiaji simu yenye nguvu inayoweza kuwafanya waunganishwe na ulimwengu, wakati wowote na mahali popote.
Msanii mahiri wa Bongo flavour Mario ambaye pia ni balozi wa Infinix NOTE 30 aliongelea uzoefu aliokuwa nao juu ya bidhaa hii, “Ninahisi kuunganishwa na hii simu nikiwa kama kijana mwenye kazi nyingi za kufanya pasipo kupoteza muda, Infinix NOTE Series imekuwa suluhisho kwangu kwa pande zote, fikiria inachukua dakika 30 tu nishati ya betri kufikia 80%, lakini pia inaniruhusu kucheza michezo wakati simu ikiendelea kujaa chaji, kuchajisha simu nyengine, licha ya kuwa na sifa hizi zote zaidi ninavutiwa na gharama yake ni rahisi kila kijana anaweza kukifikia na kutimiza malengo yake kupitia teknolojia”.