Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

BAADA YA MORRISON KUSEPA BONGO….MABOSI SIMBA WAFIKIRIA KUMSHUSHA HUYU NDUGU YAKE…

admin July 2, 2023 1:16 pm

Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Collins Opare anayekipiga ndani ya Dodoma Jiji, ameingia kwenye rada za mabosi wa Simba SC ambao wanahitaji saini yake.

Opare ni miongoni mwa mawinga wenye ushkaji na nyavu katika Ligi Kuu Tanzania Bara, aliwahi kuwafunga Young Africans walipokutana msimu wa 2022/23, huku akifunga mabao kumi kwa msimu huo.

Mtu wa karibu wa Opare, amesema kuwa, kuna ofa zaidi ya tatu zipo mezani kwake ikiwemo ya Simba SC.

“Opare ana ofa zaidi ya tatu kwa timu ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara, miongoni mwa hizo ni Simba SC ambayo ilikuwa inamuulizia tangu msimu uliopita.

“Kikubwa ambacho kwa sasa kinaangaliwa ni suala la maslahi na namna gani wanaweza kufikia makubaliano na mchezaji mwenyewe kwani kazi yake ni mpira,” amesema mtu huyo.

Afisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga, amesema kuwa: “Ni kweli wachezaji wetu walipambana kwenye ligi na kazi yao imeonakana, kuna ofa ambazo zimekuja kwa wachezaji ikiwa ni pamoja na ya Opare, hivyo ni suala la kusubiri itakavyokuwa.”

HII HAPA SABABU YA KWANINI UACHANE NA SIMU ZINGINE UNUNUE Infinix NOTE 30 PRO AU NOTE 30 VIP.. WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI ‘THANK YOU’ YA ONYANGO…AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply