Tetesi za Usajili Simba
Habari za michezo

WAKATI MASHABIKI WAKISUBIRI ‘THANK YOU’ YA ONYANGO…AHMED ALLY KAAANIKA JAMBO LILIVYO…

admin July 2, 2023 1:22 pm

Uongozi wa Simba SC umetangaza kuwa beki wao kutoka nchini Kenya, Joash Onyango Achieng, bado mali halali ya klabu hiyo, licha ya mkataba wake kubaki mwaka mmoja, huku mara kadhaa ikiripotiwa kwamba ameandika barua ya kusitisha mkataba wake huo.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema Onyango bado ataendelea kubaki Simba kwa msimu ujao.

Ameongeza kuwa bado beki huyo anahitajika katika timu hiyo, kutokana na ubora alionao wakati wakijiandaa na michuano ya kimataifa msimu ujao 2023/24.

“Hicho kinachoendelea na uvumi tu, hakuna barua yoyote tuliyoipokea kutoka kwa Onyango ya kuomba kuondoka.

“Watu wafahamu kuwa Onyango ni mchezaji halali wa Simba SC ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika msimu ujao,’ amesema Ahmed Ally.

BAADA YA MORRISON KUSEPA BONGO….MABOSI SIMBA WAFIKIRIA KUMSHUSHA HUYU NDUGU YAKE… KUHUSU ISHU YAKE YA KUSEPA YANGA…MAYELA AVUNJA UKIMYA…”HAKUNA ALIYEKUWA ANANIJUA”..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply