Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKIALIKWA MALAWI…BURUNDI WAIPA SHAVU NAMUNGO…

WAKATI YANGA WAKIALIKWA MALAWI…BURUNDI WAIPA SHAVU NAMUNGO…

Habari za Michezo leo

Namungo FC imepata mwaliko kutoka Shirikisho la Soka la Burundi (FFB), kwa ajili ya kwenda kucheza mchezo maalum wa kirafiki wa kimataifa mwishoni mwa mwezi huu, imeelezwa.

Katibu Mkuu wa Namungo FC, Ally Mkadeba, alisema wamepata mwaliko huo, lakini hawajajua wanakwenda kucheza na timu gani.

“Shirikisho la Soka Burundi limesema tuvute subira, litatufahamisha timu ambayo tutacheza nayo, kwetu tumeupokea mwaliko huo kwa mikono miwili,” amesema Mkadeba.

Aidha, katibu huyo amesema Julai 10, wanatarajia kuelekea wilayani Karatu kuweka kambi ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaoanza Agosti mwaka huu.

Amesema wamechagua kuweka kambi mkoani humo kutokana na kuwa na miundombinu mizuri ya viwanja vya mazoezi pamoja na gym za kisasa.

Wakati huo huo, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Denis Kitambi, amesema baada ya kumaliza kusaini mkataba wa miaka miwili na aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba SC, Erasto Nyoni, kwa sasa anaendelea kuwachunguza nyota wengine wa- tatu anaowahitaji.

“Baada ya kumalizana na Erasto Nyoni nipo kwenye mazungumzo ya mwisho na wachezaji ambao ninawahitaji kwa lengo la kuiongezea nguvu timu yangu,” amesema Kitambi.

Namungo imemaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kujikusanyia alama 40.

SOMA NA HII  MAKOCHA WAPISHANA KAULI ISHU YA BALEKE NA PHIRI KUACHWA PAMOJA SIMBA...ISHU HII HAPA..