Home Azam FC AZAM FC WAENDELEA KUFANYA MAKUBWA…WASHUSHA ‘KOCHA JIPYA’ LA MPIRA…NI BALAA…

AZAM FC WAENDELEA KUFANYA MAKUBWA…WASHUSHA ‘KOCHA JIPYA’ LA MPIRA…NI BALAA…

Azam FC

AZAM FC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao baada ya Julai 5, 2023 kumtambulisha kocha msaidizi kikosini hapo.

Miamba hiyo ya kusini mwa Dar es Salaam imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha Mfaransa Bruno Ferry.

Kwenye taarifa iliyotolewa na Azam Fc kupitia kurasa zake za mitandao imesema

“Tunayo furaha kuwataarifu kuwa tumeingia mkataba wa miaka mitatu na Bruno Ferry atakayekuwa kocha msaidizi”

Kocha huyo mwenye miaka 56, atasaidiana na kocha mkuu wa timu hiyo youssouph Dabo kukisuka kikosi hicho msimu ujao.

SOMA NA HII  HIZI HAPA KLABU 10 ZENYE THAMANI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI...CHAMA LAKO NAMBA NGAPI?