Home Habari za michezo YANGA WAPEWA MASHABIKI 30,000 WA KUNUNU JEZI ZAO MALAWI…RAIS SAMIA ATIA BARAKA…

YANGA WAPEWA MASHABIKI 30,000 WA KUNUNU JEZI ZAO MALAWI…RAIS SAMIA ATIA BARAKA…

Jezi mpya za Yanga msimu huu

KLABU ya Yanga  imezindua jezi zake rasmi za msimu wa 2023-24 Jijini Lilongwe kwa kuwakabidhi Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake, Rais wa Malawi Dk. Lazarus McCarthy Chakwera.

Yanga ipo Malawi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na wenyeji, Nyasa Big Bullets leo Uwanja wa Bingu Mutharika Jijini Lilongwe kuazimisha miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo.

YANGA WAPEWA USHAURI KABLA YA KWENDA MALAWI

Katika hatua nyingine, wakati Yanga SC wakiwa kwenye  mualiko wa sherehe za kuadhimisha miaka 59 ya uhuru Nchini malawi, Viongozi wa klabu hiyo wamepewa ushauri juu ya kuuza jezi zao mpya huko.

 Ushauri huo umetolewa na mbobezi wa masuala ya kibiashara ambapo amewataka Yanga kwenda  na Jezi hata 30,000 kwani  uwanja utajaa full hivyo mashabiki wa Nyasa Big Bullet na wengine watanunua jezi kwaajili ya sherehe hizo

Wakishanunua faida si kuuza bali kuitangaza klabu na kufuatiliwa kimataifa hata siku mnazindua mpya zitakuwa zinaagizwa tu. Klabu ikiwa na mvuto biashara inafanyika hata chini ya bahari

Ni heshima kubwa sana kualikwa na mtu mkuwa wa Nchi hivyo na nyinyi tumieni mwanya huo kwa kuitangaza Yanga sc katika biashara ya Jezi nje ya mipaka ya Tanzania, najua watanunua kwakuwa hawatakuwa na jezi maalumu siku hiyo na Sina shaka viingilio vitakuwa ni bure kwakuwa ni siku ya kitaifa

Mkishindwa kwenda na jezi mpya tumieni hata zile za Caf confederation Cap, fungueni tawi kule pia gaweni na kadi bila kusaahau Tangulizeni Timu ya watu kadhaa kwaajili ya kuhamasisha watu kufuata mitandao ya kijamii ya yanga sc Ili wakati wa uzinduzi wa jezi na miradi mingine wawe wanafuatilia

Manchester United inapendwa kote Duniani,inauza na kufuatiliwa sana vipi mnafikiri bila kujitoa mtaweza kuilisha Dunia?

Yani mshindwe hata hapa Africa? Inatakiwa muwe na vyanzo vya nje ya nchi na ndani ya nchi.

Je unadhani ushauri huu utaisaidia Yanga, Tuandikie maoni yako hapo chini.

SOMA NA HII  BAADA YA KURUDI UWANJANI...KAPOMBE AFUNGUKA MAZITO ALIYOYAPITIA...AMTAJA ALIYEMUOKOA...