Mkude atambulishwa yanga
Habari za michezo

RASMI…MKUDE ALAMBISHWA ASALI YANGA….MSHASHARA ATAKAOVUNA NI KUFRU TUPU AISEE…

admin July 12, 2023 9:02 pm

Club ya Yanga imetangaza rasmi kuwa imemsajili aliyekuwa mchezaji Mwandamizi wa Simba SC Jonas Gerald Mkude kama Mchezaji huru baada ya Mkataba wake na Simba SC kumalizika.

Huu unakuwa ni usajili wa tatu wa Yanga msimu huu baada ya kumsajili Kibabage na Gift Fred kutoka SC Villa ya Uganda.

Mkude amejiunga Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezewa mwaka wa pili, ambapo atakuwa akilipwa mshahara wa milioni 10 pamoja na posho zingine.

Aidha mbali ya kusaini mkataba huo, Mkude pia atalipwa pesa za usajili zaidi ya milioni 50 , huku akihaidiwa mambo mazuri zaidi kama atakipiga kweli kweli.

Mkude ameondoka Simba SC baada ya kuitumikia kwa miaka 13 toka alipojiunga nayo 2010.

KUSANYA MAOKOTO YAKO MAPEMA KUPITIA 40 LUCKY SEVENS YA MERIDIANBET… WAKATI YANGA WAKITAMBA NA FAINAL YA SHIRIKISHO…CAF KUIMWAGIA SIMBA MABILIONI…ISHU IKO HIVI..

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply