Habari za michezo

KUMBE MKUDE SIO JEZI NAMBA 6 WA YANGA, ALLY KAMWE AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU NAMBA SITA NA UJIONWAKE ISHU IKO HIVI

Staff Desk July 15, 2023 9:35 am

Joto likiwa linazidi kupanda kwa Mashabiki wa Soka nchini wakitaka kumjua mchezaji atakaeva jezi namba 6 ya Yanga ambayo ilikuwa ikivaliwa na Feisal Salum alietimkia Azam FC.

Afisa habari wa Yanga Ally Kamwe ameweka wazi siku ya utambulisho wa mchezaji huyo na sifa zake kuelekea kilele cha Siku ya Mwananchi ambayo itakuwa Julai 22.

“Hadi kufika Jumanne, tutakuwa tumemaliza zoezi zima la utambulisho wa sajili zetu.Watu wanafikiri utambulisho wa Jonas Mkude ndio namba 6 tuliyoisema, bado namba sita hajatangazwa,”

“Yeye atakuwa ni mtu wa mwisho kutangazwa, siku akitangazwa wananchi wataingia mtaani kufurahia, itakuwa ni kama sikukuu ya mwaka mpya.Tukimtambulisha mafataki yatapigwa, ngoma zitapigwa, nyimbo zitaimbwa kila pande ya nchi hii watu watafurahi,”

“Tutamtambulisha kabla ya wiki ya Wananchi, Kaizer Chiefs wao watakuwa watu wa mfano kuwasimulia watu wengine kuhusu unyama na ukatili alionao huyu jezi namba 6.”

Mpaka sasa Yanga imeshafanya usajiliwa wachezaji watano wazawa wawili na wa kigeni watatu ambao ni Nickson Kibabage, Jonas Mkude (wazawa) na wa Kimataifa ni Beki Gift Fred, Maxi Mpia Nzengeli na beki Yao Khouassi

WAKATI SIMBA , YANGA WAKIENDELEA KUTANGAZA WACHEZAJI WAKE WAPYA…. WASENEGAL WA AZAM WATAMBA TUNISIA HII SASA SIFA, UNAJUA KWANINI? SIMBA KAMA INATAKA KUKOMOA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply