Home Habari za michezo MORRISON BAADA YA KUTEMANA NA YANGA, BOSI WA SFG AFUNGUKA HAYA

MORRISON BAADA YA KUTEMANA NA YANGA, BOSI WA SFG AFUNGUKA HAYA

BOSI wa Singida Fountain Gate (SFG), Japhet Makau amesema usajili waBernard Morrison ni suala la muda tu na mashabiki wakae kwa kutulia kwani mambo mazuri yanakuja zaidi msimu huu.

Morrison alipewa Thank You na Yanga na inadaiwa tayari amemalizana na SFG kwa ajili ya kuitumikia msimu ujao wa Ligi Kuu Bara na mashindano ya kimataifa ambapo watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti katika, Makau alisema kuwa; “Ishu ya Morrison tusubiri Agosti 2, ambapo tutatambulisha kikosi chetu.”

Kuhusu usajili wa wachezaji wapya akiwemo beki wa zamani wa Simba, Joash Onyango raia wa Kenya alisema matumaini yao ni makubwa na wana imani watafanya vizuri na watakuwa msaada mkubwa kwao.

“Kuna tofauti timu moja na timu nyingine, huwezi kusema mchezaji kama Onyango ameachwa, sisi tuna imani nae na atafanya vizuri na atacheza kwa jinsi ambavyo kocha atamtumia, naamini wachezaji tuliowasajili wanaenda kufanya vizuri kwenye timu yetu,” alisema Makau.

Bosi huyo alisema wamepanga kucheza michezo mitatu ya kirafiki kabla ya kuanza Ligi Kuu ambayo watacheza Singida, Tanga na Arusha.

“Tutacheza Arusha ambako ndiko timu imeweka kambi, tutaenda kucheza Singida Agosti 2 mwaka huu katika siku yetu na tutaenda Tanga kucheza mechi ya Ngao ya Jamii,” alisema Makau.

Kuhusu maandalizi ya timu hiyo, Makau alisema yanaendelea vizuri jijini Arusha na wamepanga kutambulisha majembe yao Agosti 2 mwaka huu katika sherehe zinazotarajiwa kufanyika katika Uwanja Liti mkoani Singida.

“Unapofanikiwa unatengeneza ushindani mkubwa msimu unaofuata washindani wanakuangalia kwa umakini tumejipanga na malengo yetu ni kuwa katika nafasi tatu za juu.”

SOMA NA HII  BAADA YA KUKIWASHA KWENYE CAF ....YANGA WABARIKI PACOME, MAXI KUPIGWA BEI...

1 COMMENT