Habari za michezo

YANGA HII YA GAMONDI SIO POA CHEKI BALAA LAKE

Staff Desk July 26, 2023 10:51 am

CHINI ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Yanga inaendelea na mazoezi kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Ni AVIC Kigamboni Yanga imeweka kambi ikiwa na maingizo ya wachezaji wapya pamoja na wale waliokuwa katika kikosi hicho msimu wa 2022/23.

Tayari Yanga imeshafanya utambulisho wa wachezaji wao ikiwa ni pamoja na Nickson Kibabage ambaye alikuwa anakipiga ndani ya Singida Fountain Gate.

Kwa wazawa wapo Dickson Job beki wa mpira mwenye tuzo ya beki bora ndani ya ligi msimu wa 2022/23.

Katika Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Asas FC ambapo itaanzia ugenini na itamalizia nyumbani.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Agosti 18 2023.

GAMONDI AANZISHA VITA HII YANGA, MASTAA WAHAHA AHMED ALLY AFUNGUKA KILA KITU KUHUSU VIINGILIO VYA SIMBA DAY MAMBO HADHARANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply