Azam FC

Azam FC Yamtambulisha Rasmi Beki Henri Stanic ‘The Destroyer’ Kutoka Stellenbosch

Vardo July 17, 2026 7:27 pm

Klabu ya Azam FC imeendelea kutikisa soko la usajili nchini baada ya kukamilisha rasmi usajili wa beki wa kati raia wa Ubelgiji, Henri Stanic, akitokea Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa 2026-2027.

Beki huyo mwenye mwili nyumba, anayefahamika zaidi kwa jina la utani la ‘The Destroyer’, ametua Chamazi akiwa na dhamira kuu ya kuiongezea nguvu safu ya ulinzi ya matajiri hao wa kuoka mikate ili kurejesha heshima ya klabu hiyo kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.

Kwanini Stanic Alichagua Azam FC?

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa, Stanic ameweka wazi kuwa haikumpa shida kufanya maamuzi ya kujiunga na miamba hiyo ya soka la Tanzania, kwani alikuwa akifuatilia kwa ukaribu ukuaji wa Ligi Kuu ya NBC.

“Nadhani haikuchukua muda mrefu kufanya uamuzi. Nilijua kuhusu Ligi Kuu Tanzania na ushindani wake. Ni moja ya ligi zinazokuwa kwa kasi na niliona huu ndiyo wakati sahihi kwangu kujaribu changamoto mpya,” alisema Stanic.

Ameongeza kuwa kuvutiwa kwake na ushindani wa timu kubwa hapa nchini ndio kigezo kilichomfanya atamani kuja kuonyesha uwezo wake: “Ninapenda kushindana katika mazingira yenye ushindani mkubwa. Hilo ndilo lililonivutia zaidi. Ninaamini kujiunga na Azam kutanifanya niendelee kukua kama mchezaji na wakati huohuo kuisaidia timu kufikia malengo yake.”

Uzoefu na Sifa za ‘The Destroyer’

Stanic anajiunga na Azam FC akitokea Stellenbosch FC, timu ambayo imekuwa mwiba mchungu nchini Afrika Kusini ikichuana vikali na vigogo kama Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates.

Akiwa huko, alijizolea sifa kibao kutokana na:

  • Uimara mkubwa kwenye ukabaji wa ana kwa ana.

  • Uwezo wa juu wa kucheza mipira ya kichwa (juu).

  • Utulivu mkubwa wa kuanzisha mashambulizi kutokea safu ya nyuma.

  • Uongozi thabiti uwanjani alioupata kutokana na kucheza soka barani Ulaya na Afrika Kusini.

Matajiri wa Chamazi Kurekebisha Makosa

Usajili huu unakuja kama sehemu ya mpango wa uongozi wa Azam FC kufanya maboresho makubwa kwenye kikosi chao. Msimu uliopita, timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kupoteza fainali ya Kombe la CRDB dhidi ya Simba SC—matokeo ambayo hayakuwaridhisha mashabiki na uongozi wao.

Ujio wa Henri Stanic unatarajiwa kuleta utulivu na kuongeza ushindani mkubwa kwenye ngome ya ulinzi ya Azam FC ili kuhakikisha wanarudi kwa nguvu kuwania mataji yote msimu huu.

Odds Kubwa Zinakungoja Mechi za Leo Donald Trump Kuhudhuria Fainali Ya Kombe La Dunia 2026