Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUZINDUA UZI WAO JANA…HII HAPA TAARIFA MPYA KUHUSU JEZI...

BAADA YA YANGA KUZINDUA UZI WAO JANA…HII HAPA TAARIFA MPYA KUHUSU JEZI ZA SIMBA…

Habari za Simba leo

Kampuni ya Sunderland imesema itazindua kwa pamoja jezi zote za Klabu ya Simba za mashindano ambayo wanashiriki kwa msimu wa 2023/24.

Jezi hizo ni za CAF Super League, Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’, Ligi Kuu ya Wanawake na Ligi ya Vijana.

Akizungumza na Azam TV, mzabuni aliyeshinda zabuni ya kutengeneza jezi za Simba SC, Sunday Omar amesema tayari jezi hizo zipo nchini na klabu ndio watasema wanazindua lini.

Amemuomba Waziri wa Biashara na Viwanda, Mkurugenzi wa FCC, Polisi na mamlaka nyingine kusaidia kudhibiti jezi ‘Fake’ ili timu zinufaike na mapato yanayotokana na mauzo ya jezi zao.

Sunderland iliingia mkataba Sh bilioni 4 na Simba SC baada wa miaka miwili wenye thamani ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia nao miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh bilioni 2.

SOMA NA HII  HAWA HAPA MASTAA MUHIMU WA YANGA WATAKAOKOSEKANA MECHI NA MAZEMBE...DIARRA NDANI...