Home Uncategorized AZAM FC V ALLIANCE NI VITA YA KISASI KESHO

AZAM FC V ALLIANCE NI VITA YA KISASI KESHO

KIKOSI cha Azam FC, kesho, Machi 7, kitakuwa Uwanja wa Taifa kumenyana na Alliance ya Mwanza kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Azam FC itashuka uwanjani ikiwa na kumbuku ya kupoteza mchezo wake uliopita mbele ya Simba huku Alliance FC ikitoka kupoteza mbele ya Ruvu Shooting.

Alliance ilifungwa na Ruvu Shooting bao 1-0 Uwanja wa Mabatini huku Azam FC ikipoteza mbele ya Simba kwa kufungwa mabao 3-2.

Mechi hiyo itakuwa ni ya kisasi kwa Alliance ambao mchezo wa kwanza uliochezwa Nyamagana walichapwa mabao 5-0 huku Obrey Chirwa akisepa na mpira jumlajumla baada ya kufunga hat trick.

Nyota wa Azam FC, Anderw Simchimba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mechi zote watakazocheza huku nyota wa Alliance Sameer Vincent amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI IJUMAA