Home Habari za michezo HIVI NDIVYO YANGA ‘WALIVYOMFINYA’ MORRISON KUHUSU TABIA ZAKE ZA AJABU AJABU…AKIZINGUA HANA...

HIVI NDIVYO YANGA ‘WALIVYOMFINYA’ MORRISON KUHUSU TABIA ZAKE ZA AJABU AJABU…AKIZINGUA HANA CHAKE…


Imebainika kwamba, mkataba aliopewa winga Bernard Morrison raia wa Ghana ndani ya Yanga, umemfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wenye nidhamu kubwa kikosini hapo na kuwa mfano wa kuigwa kwa wenzake.

Morrison ambaye amerejea Yanga msimu huu akitokea Simba, katika mkataba mpya, amewekewa vipengele vingi vinavyombana ikiwemo kutokuwa mtovu wa nidhamu.

Chanzo chetu kutoka Yanga, kimesema kwamba, mabadiliko ya nidhamu ya Morrison yamekuja kwa haraka kutokana na kubanwa na baadhi ya vipengele alivyowekewa kwenye mkataba wake huo wakati akijiunga na timu hiyo msimu huu.

“Watu wengi wameshangazwa na kitendo cha Morrison kumkabidhi mpira Djuma Shaban ili apige penalti dhidi ya Azam, wengi walifahamu kwamba kutokana na jeuri yake angepiga yeye.

“Lakini wasichokifahamu ni kwamba, sasa hivi Morrison ni kati ya wachezaji wa mfano wa kuigwa, maana vipengele alivyowekewa kwenye mkataba vinamfanya awe hivyo.

“Mkataba aliosaini msimu huu Yanga, ulikuwa ni wa gharama kubwa, sana jambo ambalo limewafanya viongozi wake kumpa vipengele vya kumbana endapo akisababisha kosa lolote ndani ya mchezo au kuchelewa kuingia kambini, anaweza kukatwa zaidi ya shilingi milioni tatu.

“Mbali na hivyo, hata akionekana amechelewa kuingia kambini au kufanya mahojiano na waandishi bila ruhusa ya uongozi wake anaweza kupoteza zaidi ya shilingi milioni 5, kwenye mshahara wake.

“Pia akivunja mkataba, anaweza kujikuta akilipa nusu au zaidi ya fedha aliyopewa wakati akiusaini,” kilisema chanzo hicho.

Akimzungumzia Morrison, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amesema: “Morrison kwa sasa ni mfano wa kuigwa linapokuja suala la utii na nidhamu.”

SOMA NA HII  HUYU HAPA STARIKA LA KUFUNGA KUTOKA TP MAZEMBE ANAYETAJWA KUTUA SIMBA MSIMU UJAO...NI BALAAHA NA NUSU...