Home Habari za michezo WASUDANI WAIRUDISHA YANGA KWA MKAPA….WAKIPETA HATUA HII KUKUTANA TENA HAPO HAPO…

WASUDANI WAIRUDISHA YANGA KWA MKAPA….WAKIPETA HATUA HII KUKUTANA TENA HAPO HAPO…


MCHEZO wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya wenyeji Zalan FC kutoka Sudan Kusini dhidi ya Yanga utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam tofauti na mwanzo ulivyopangwa kuchezwa Azam Complex.

Zalan imeamua kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwenye mchezo huo kutokana na viwanja vyake nchini Sudan kukosa hadhi ya kuchezea mashindano.

Mchezo huo wa hatua za awali utakaopigwa Jumamosi ya Septemba 10 unaipa faida Yanga kwa sababu hata mechi ya marudiano itakayochezwa Septemba 17, uwanja huo huo utaendelea kutumika kwani wao ndio watakaokuwa wenyeji.

Zalan ambao ndio mabingwa watetezi wa Ligi ya Sudan wanaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kocha mpya baada ya Klabu hiyo Agosti 18 kumtangaza, Baping Alliab kukinoa kikosi hicho akitokea Al Hilal Wau ya Sudan Kusini akichukua nafasi ya Richard Ola.

Mshindi wa jumla baina ya klabu hizo atapambana na mshindi kati ya Mabingwa wa Ligi ya Ethiopia St. George au Al Hilal ya Sudan.

SOMA NA HII  KWA KOSI HILI...WAARABU WATASHANGAA..MABOSI SIMBA WATENGA MAMILION...MAYELE ABAMBWA AKITOA SIRI ....