Home Uncategorized SIMBA BANA, YATIMIZA 4G MBELE YA ALLIANCE YA MINZIRO

SIMBA BANA, YATIMIZA 4G MBELE YA ALLIANCE YA MINZIRO


SVEN Vandenbroeck leo ameongoza kikosi chake cha Simba kupata ushindi wa mabao 4-1 mbele ya Alliance FC, iliyo chini ya Felix Minziro.

Alliance leo ilianza kwa kasi ambapo ilifunga bao la kuongoza dakika ya 27 kupitia kwa faulo iliyopigwa na Israel Mwenda akiwa nje ya 18 iliyomshinda mlinda mlango Beno Kakolanya.

Jonas Mkude kiungo wa Simba alifunga bao la kusawazisha dakika ya 45 kwa shuti kali akiwa nje ya 18 lililozama kimiani na kuwafanya Simba na Alliance kwenda mapumziko wakiwa wametoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

 Kipindi cha pili Simba iliandika bao la pili kupitia kwa Meddie Kagere dakika ya 58 na iliwachukua dakika tano kuandika bao la tatu kwa Simba ambapo Clatous Chama alifunga kwa kutumia mpira wa adhabu akiwa nje ya 18 na ulizama nyavuni.

Msumari wa mwisho kwa Simba ulipachikwa na Hassan Dilunga ambaye kipindi cha kwanza alikosa bao la wazi kwa kupaisha juu mpira alifunga bao hilo dakika ya 72 na kuhitimisha jumla ya mabao 4-1. 

Ushindi huo unaifanya Simba kujikita kileleni ikiwa na jumla ya pointi 41 ikiwa imecheza jumla ya mechi 16 za Ligi Kuu Bara.

Sven amesema kuwa hesabu zake ni kuona anapata pointi tatu kwenye mechi zake zote zilizobaki na atayafanyia kazi makosa huku Minziro akisema kuwa matokeo waliyopata ni mabaya.

SOMA NA HII  GAMONDI AWATULIZA PRESHA WACHEZAJI WA YANGA.......... MECHI NI YETU HII