Home Habari za michezo BAADA YA TETESI ZA KUSEPA KWAKE KUZAGAA LEO….CEO WA YANGA KASEMA NENO...

BAADA YA TETESI ZA KUSEPA KWAKE KUZAGAA LEO….CEO WA YANGA KASEMA NENO HILI TU MOJA…

Habari za Yanga leo

Ofisa Mtendaji wa Klabu ya Yanga, Andre Mtine amekanusha taarifa za kwamba ameondoka ndani ya klabu hiyo.

Taarifa zilizokuwa zinasambaa mitandaoni ni kwamba Mtine raia wa Zambia ameondoka ndani ya Klabu ya Yanga baada ya kutofautiana na uongozi wa klabu hiyo kuhusu masuala ya fedha.

“Hapana sijaondoka Yanga sc ila nilikuwa likizo, na narudia leo Tanzania majira ya saa 18:10 jioni,” amesema Mtine.

Taarifa za kuondoka kwa Mtine yanga zilisambazwa awali na mtangazaji wa Clouds FM, Sharfii Dauda kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo hakuandika chanzo cha taarifa hizo.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa Mtime amekuwa na sintofahamu na Rais wa Yanga, Eng Hersi ambapo chanzo kikidaiwa ni yeye kuingiliwa majukumu yake ya kiutendaji na Rais huyo.

Mtine alijiunga Yanga mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea kwao nchini Zambia, ambapo alikuwa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa CEO wa klabu hiyo Msauzi Senzo Mazingiza ambaye alijiengua Yanga.

Senzo ambaye alijiunga na Yanga akitokea Simba, alikokaa kwa msimu mmoja na nusu, kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Ligi Kuu ya Botswana.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA YANGA KESHO....DODOMA JIJI WAWEKEWA MIL 30 MEZANI...