Home Habari za michezo KWA YANGA HII, TABU IKO PALEPALE

KWA YANGA HII, TABU IKO PALEPALE

Habari za Yanga

KAMA vipi irudiwe! huwezi kusema neno lingine baada ya Yanga jana kufanikiwa kuonyesha kiwango kizuri ilipoichapa Kaizer Chief bao 1-0 kwenye mchezo wa kileleni cha siku ya Mwananchi uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa.

Huu ulikuwa mchezo muhimu kwa Yanga ambao ulikuwa maalum kwa ajili ya kutazama kikosi chao kipya kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika, Ngao ya Jamii na hata Kombe la Azam Federation.

Katika tamasha hilo ambalo hakuna neno lolote lililozungumzwa kuhusu mshambuliaji Fiston Mayele kama tayari anaondoka au la, Kennedy Musonda aliwaonyesha mashabiki wa Yanga kuwa anaweza kuziba pengo la Mcongo huyo bila shida.

Musonda ambaye alionekana kupania kwenye mchezo huo alionyesha kiwango cha juu dakika 45 za kwanza baada ya kufanikiwa kufunga bao safi katika dakika ya 45 kwa pasi safi kutoka kwa Maxi Nzegela.

Kipindi cha kwanza kocha wa Yanga, Gamondi aliwaanzisha wachezaji watano wageni, Jonas Mkude, Kibabage, Maxi Nzengeli na Muhalatse Makudubela ambao walionyesha kiwango cha hali ya juu sana, zaidi katikati mwa kiwanja.

Hata hivyo, pamoja na wachezaji wengine kutakata, lakini mashabiki wa Yanga watakuwa wameondoka na jina la Mkude ambaye alijiunga nao akitokea Simba kutokana na kiwango cha juu ambacho alikionyesha.

Gift Fred ambaye aliingia kipindi cha pili naye hakuwa nyuma kwenye ubora wake kwani alifanikiwa kuwateka mashabiki wa Yanga kutokana na kuonyesha kiwango kizuri kwa dakika alizocheza.

Huu ulikuwa mchezo wa pili Yanga wanashinda kwenye siku ya Mwananchi baada ya kupoteza michezo miwili, walitoka sare mmoja kuanzia wameanza tamasha hilo.

Hata hivyo, mashabiki wa Yanga bado wana hamu ya kumuona Pacome Zouzoua ambaye hakucheza kabisa.

SOMA NA HII  MZIKI HUU WA YANGA BADO HAMJASEMA...... AL MAREIKH HAWAAMINI MACHO YAO