Home Habari za michezo LUIS MIQUISSONE ATINGA UTURUKI KIBABE AKUTANA NA WAMBA HAWA, HATARI TUPU

LUIS MIQUISSONE ATINGA UTURUKI KIBABE AKUTANA NA WAMBA HAWA, HATARI TUPU

Habari za Simba

LUIS Miquissone kiungo wa Simba baada ya kujiunga na wachezaji wenzake nchini Utuki ameanza mazoezi tayari kwa ajili ya msimu mpya wa 2023/24.

Kiungo huyo wa Simba alisepa hapo 2021 na kuibukia Al Ahly ambapo huko hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza kutokana na ushindani wa namba.

Hivi karibuni alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mabosi wake wa Al Ahly ambapo tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa anaweza kuibukia Azam FC ama Yanga.

Yanga walikuwa wanatajwa kutokana na kutambua uwezo wa kiungo huyo alipokuwa ndani ya Simba pamoja na Azam FC nao walimuona alipokuwa akivuja jasho.

Mwisho dili la Yanga na Azam halikujibu kama tetesi zilivyokuwa zinaeleza na badala yake amerejea kwa mara nyingine dani ya Simba.
Kiungo huyo amesema; β€œNimerejea ndani ya Simba kwa mara nyingine kufanya kazi kwa mara nyingine tena nina amini tutafikia mafanikio na malengo yetu kwa kuwa kila kitu kinawezekana,” .

Anaungana na viungo wengine ikiwa ni mshikaji wake Clatous Chama, Peter Banda ambaye anavaa jezi namba 11 aliyokuwa anaivaa zama zile alipokuwa ndani ya Simba.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA AWAPIGA PANGA WACHEZAJI...YANGA SC "TUNAZITAKA POINTI ZA MAZEMBE