Home Habari za michezo WAKATI YANGA WAKITAMBA NA FAINAL YA SHIRIKISHO…CAF KUIMWAGIA SIMBA MABILIONI…ISHU IKO HIVI..

WAKATI YANGA WAKITAMBA NA FAINAL YA SHIRIKISHO…CAF KUIMWAGIA SIMBA MABILIONI…ISHU IKO HIVI..

Habari za Simba

SHIRIKISHO la Soka Barani Afrika(CAF) limebadilisha jina la mashindano yake mapya, lakini Rais wake,Patrice Motsepe amesisitiza kwamba yatakuwa na neema kubwa ya mkwanja Simba ikiwa mshiriki pekee wa Cecafa hadi sasa.

Awali mashindano hayo ambayo pendekezo la awali ni kushirikisha timu nane, yanaanza Oktoba yalipangwa kuitwa Super League lakini sasa yatajulikana kama African Footbal League (Ligi ya Soka ya Afrika).

“Marafiki zetu wa Ulaya walitushauri kutotumia ‘Super League’ kutokana na uhusiano mbaya na ile ya kwao ilivyofeli majuzi,” alisema.

Motsepe ameeleza kuwa michuano hiyo itashirikisha timu nane pekee, zikiwemo timu zilizofuzu kwa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023 Ahly ya Misri, Wydad Casablanca ya Morocco, Esperance ya Tunisia, na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Nyingine ni TP Mazembe ya DR Congo, Enyimba ya Nigeria, Simba ya Tanzania na Petro Atletico ya Angola.

“Tumeamua kubadilisha jina la Super League kuwa Ligi ya Soka ya Afrika,” Motsepe alisema katika mahojiano na televisheni ya beIN Sport ya Qattar.

“Ligi ya Soka ya Afrika itaanza Oktoba kama ilivyokuwa imepangwa, itakuwa ligi bora zaidi kutokana na ukubwa ya zawadi,” alisema Motsepe na kuongeza kuwa maelezo zaidi ya michuano hiyo yatafafanuliwa hivikaribuni nchini Ivory Coast.

Bingwa wa michuano hiyo atapewa Bil 28. Klabu zitatoka kwenye kanda tatu za Afrika ambapo ni Kaskazini, Kati/Magharibi, Kusini/mashariki.

SOMA NA HII  KUHUSU ISHU YA MBRAZILI KUFUKUZWA....KIGOGO SIMBA AVUNJA UKIMYA...ATAJA MSIMAMO YA KLABU...