Home Habari za michezo WALIOIVURUGA REKODI YA YANGA WAPO SANA

WALIOIVURUGA REKODI YA YANGA WAPO SANA

NYOTA wawili walioivuruga rekodi ya Yanga kufikisha mechi 50 bila kufungwa ndani ya ligi bado wapo ndani ya Ihefu baada ya kuongezewa mkataba.

Yanga ilicheza mechi 49 bila kufungwa kwenye mechi za ligi ilipokutana na Ihefu ilishindwa kupata sare ama ushindi zaidi ya kufungwa mabao 2-1 na kutibua rekodi hiyo iliyoandikwa na Yanga.

Wafungaji kwenye mchezo huo ni Lenny Kissu na Nivere Tigere ambao wote wanauhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao.

Peter Andrew Ofisa Habari wa Ihefu amesema: β€œMlinzi bora Lenny Kissu naye atakuwepo mbali na huyo pia kiungo Nivere Tigere Mr Freekik ataendelea kubaki Uwanja wa Highland Estate.”
Wengine ambao wataendelea kubaki Ihefu ni nahodha Rafael Daud, Jaffary Kibaya na wengine wapya wanatarajiwa kutambulishwa hivi karibuni.

Mbali na hao watibuaji rekodi ya Yanga pia Rashid Juma, Juma Nyosso nao wataendelea kubaki ndani ya timu hiyo.

SOMA NA HII  WAKATI MASHABIKI WA GEITA GOLD WAKISEMA WATAISUSA TIMU....'FEI TOTO' NA FARID WAWAANGUKIA YANGA....